Watumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza wapatiwa mafunzo ya mfumo wa uhamisho
Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki hii wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa uhamisho unaojulikana kama ESS yaani(Employment Self Service) utaratibu unaotumika sasa kuomba uhamisho kupitia mfumo huo.
Akitoa mafunzo hayo kwenye ukumbi wa Ofisi ya mkuu wa mkoa,Afisa TEHAMA Mkoa wa Mwanza Joseph Chali amesema watumishi wote ni lazima wajisajili kwenye mfumo huo kwasababu kwa njia moja ama nyingine anaweza kufikiria kuhama siku moja,hata Mkuu wa Taasisi.
"Katika mfumo huu kuna vipengere mbalimbali ambapo hivyo vyote lazima uwe navyo ili kukamilisha uhamisho wako ambavyo ni CV iliyohuishwa Taasisi unayotaka kuhamia na kuonyesha sababu ya kutaka kuhama",amefafanua Chali wakati akizungumza na watumishi hao.
Wakati huohuo Kampuni ya mawasiliano ya HALOTEL tawi la Mwanza imetoa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa ya bidhaa yake mpya ijulikanayo kama M2M ambayo ni laini maalum kwa watumiaji wakubwa wenye matumizi ya internet.
Afisa Habari wa Kampuni hiyo, Hassan Ally amebainisha mbali ya bidhaa hiyo yenye lengo la kumrahisishia mawasiliano ya kidunia mteja wake,Kampuni ya HALOTEL ina miundombinu ya kisasa ya mawasiliano ya simu yenye idadi kubwa ya minara ipatayo 3000 iliyounganishwa na mkongo wa KM 20,000 kuzunguka nchi nzima.
Ameongeza kuwa Kampuni hiyo ina lengo la kuwa mtoaji wa gharama ya chini zaidi ya huduma na bidhaa zake na kutoa kipaumbele kwa asilimia 95 kwa watu waishio vijijini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.