Hii ndio hifadhi iliyo ndogo kuliko zote nchini Tanzania na Afrika ya mashariki.Jina la hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha saa Nane kinachopatikana katika ziwa Victoria katika mkoa wa Mwanza kimetokana na mtanzania aliyekuwa mvuvi na mmiliki wa kisiwa hiki aliyejulikana kama Mzee saa Nane Chawandi ambaye aliachia eneo hili la kisiwa kwa serikali ya Tanzania baada ya yeye mzee saa Nane Chawandi kufidiwa gharama za eneo lake na serikali katika miaka ya 1960.
Mara moja serikali ya Tanzania ikalianzisha eneo hili la kisiwa kama bustani ya Wanyamapori ya kwanza kabisa nchini Tanzania katika mwaka wa 1964.Malengo ya serikali ya wakati wa kipindi kile ilikuwa ni kuendeleza uhifadhi endelevu wa eneo lenyewe pamoja na kuhamasisha na kuelimisha elimu ya utalii na mazingira kwa watanzania wenyewe na wageni kutoka nje ya nchi lakini vilevile ilikuwa na kutoa burudani kwa wakazi wa mji na mkoa wa mwanza na sehemu nyinginezo za mbali.
HISTORIA YAKE
Kati ya mwaka 1964 mpaka 1966 shirika la hifadhi za Taifa nchini Tanzania liliwasafirisha na kuwaleta wanyamapori wa aina mbalimbali katika kisiwa hiki cha saa nane kutoka katika maeneo mbalimbali ya uhifadhi nchini Tanzania.Wanyamapori hawa ilikuwa pamoja na nyati(mbogo),pongo,digidigi au saruya,Tembo(ndovu),pofu, swala pala,Faru,nyamera,ngiri pamoja na nyumbu.Wanyamapori wengineo ni pamoja na pundamilia,nyani,twiga,nungunungu pamoja na mamba.Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba hii ndio hifadhi ya pili inayopatikana katika ziwa Victoria katika mkoa wa mwanza baada ya hifadhi ya Taifa ya visiwa vya Rubondo ambavyo navyo pia vinapatikana katika mkoa wa Mwanza.
MAANDALIZI YA USAFIRI:
Mipango na utaratibu wa safari ya matembezi ya kutembelea kisiwa cha saa Nane kwa njia ya usafiri wa majini wa boti zenye injini huandaliwa kwa kutoa taarifa katika makao makuu ya hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha saa Nane yanayopatikana capri point katika wilaya ya nyamagana.
KUANZISHWA KWAKE:
Hifadhi hii ya Taifa ya kisiwa cha saa Nane imeanzishwa mwaka 2012 baada ya kupitishwa na kudhibitishwa na sheria za bunge la Tanzania katika mwezi oktoba,2012.
ENEO LAKE:
Mpaka hivi sasa hifadhi hii ya Taifa ya kisiwa cha saa Nane ina ukubwa wa eneo la kilomita za mraba 0 nukta 7 ambapo inajumuisha kwa pamoja eneo la nchi kavu na majini.Lakini hata hivyo katika mipango ya baadaye ya kuliongeza eneo hili ukubwa wake Itahusisha visiwa viwili vidogo vya Chankende kubwa na chankende ndogo katika upande wa kusini kijiografia na kulifanya eneo hili la kisiwa cha saa Nane kufikia ukubwa wa kilomita za mraba 1nukta 32. Ikumbukwe na ieleweke ya kwamba hii ndio hifadhi pekee iliyo ndogo nchini Tanzania na Afrika ya mashariki kwa hivi sasa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.