Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella amesema kuwa licha ya maonesho ya nane nane kugawanyika Kikanda, yameimalika zaidi Kanda ya Ziwa Magharibi.
Mhe.Mongella ameyasema hayo kwenye kilele cha maonesho ya nane nane yaliyofanyika viwanja vya Nyamhongolo jijini Mwanza.
Amesema, Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita ni Kanda nyeti sana huku akisifia umati wa watu uliojitokeza kwenye maonesho hayo.
“ Pamoja hapa sio maadhimisho ya Kitaifa lakini kila mtu anayepita hapa anaenda Bariadi anauliza pale ni vipi, siku mkileta hapa kitaifa ndo mtajua mchezo huu ukoje”alisema Mhe. Mongella
Aidha ameipongeza Kanda ya Ziwa Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga, walikuwa kanda moja kabla ya kutenganishwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel amezitaka Halmashauri kuendeleza elimu iliyotolewa kwenye maonesho hayo kwa kuwapa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu wanaopewa mikopo na halmadhauri .
Awali akisoma taarifa ya kamati ya maandalizi, Mwenyekiti wa kamati hiyo Emil Kasagara alisema, jumla ya washiriki 399 wameshiriki kutoka nyanja zote.
Akiwawakilisha wakulima, Mkulima wa vitunguu Masumbuko Kulwa amesema maonesho ya nane nane yamemuongezea uelewa juu ya zao hilo huku akitaka makampuni yanayohusika na kilimo yasisubiri tu sikukuu ya wakulima ndiyo yatoe elimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.