Kongamano la Nne la Kitaifa la wiki ya ufuatiliaji Tathmini na kujifunza (MEL) linalohusisha wataalamu kutoka nchi 18 wakiwemo Wataalamu wa ndani na wanazuoni liatarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza kuanzia Septemba 10 hadi 13, 2025.
Akizungumza leo Septemba 09, 2025 na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema kongamano hilo ni jukwaa la kitaifa linalowakutanisha washiriki takribani 1000 ikiwa ni wadau mbalimbali wa maendeleo.
Ameongeza kuwa kongamano hilo limelenga kubadilishana uzoefu, kujifunza na kuimarisha mbinu bora za ufuatiliaji na tathmini katika utekelezaji wa sera, mipango na miradi ya maendeleo.
Aidha Mhe. Mtanda amesema kupitia ufuatiliaji na tathmini miradi ya maendeleo nchini imeweza kutekelezwa kikamilifu na kwa ufanisi huku akitolea mfano miradi ya kimkakati na ya maendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea Mkoani Mwanza yenye thamani ya shilingi Trilioni 5.6.
"Miradi hiyo imewezesha uwekezaji mkubwa katika kujenga uchumi na kuboresha hali za maisha ya watu ikiwemo kuboresha miundombinu ya kiuchumi na kijamii".
Kongamano hilo kwa mwaka huu litafanyika Wilayani Ilemela Mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa Malaika Beach Resort chini ya kaulimbiu "Ufuatiliaji na Tathmini Unaongozwa na Jamii: Kujenga Uwezo wa Ndani na Kuimarisha Umiliki wa MEL kwa Matokeo Endelevu".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.