Maafisa Ushirika Kanda ya Ziwa na Kigoma wamejengewa uwezo wa ukaguzi na usimamizi wa vyama vya ushirika ili kuweza kuwa na udhibiti mzuri wa vyama hivyo huku wakitakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwakuzingatia sheria, kanuni na taratibu zote zinazosimamia majukumu yao.
Akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel ameeleza kuwa Serikali haitomfumbia macho Afisa Ushirika yeyote au Mtendaji yeyote wa Serikali atakayebainika kuvihujumu Vyama vya Ushirikka kwa namna yeyote ile.
Anasema Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuiendeleza sekta ya Kilimo kwa lengo la kumsaidia mkulima mmoja mmoja kwani kilimo kitakuwa na manufaa makubwa endapo mazao yanayozalishwa yana soko la uhakika na wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati.
Anasema Ili kufanikisha azma hiyo, serikali imeendelea kuhamasisha Wananchi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujiunga au kuanzisha vyama vya Ushirika katika maeneo yao ambapo serikali itaendelea kuvisimamia vyama hivyo ili viweze kuwasaidiawakulima katika kuzalisha na kuuza mazao yao, kuwalipa fedha kwa wakati na kusaidia upatikanaji wa pembejeo kwa wakati.
Anaeleza kuwa taarifa za ukaguzi unaofanywa na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) zimekuwa zikionesha madhaifu makubwa kila mwaka ambao wakati mwingine ni kutokana na usimamizi usioridhishawa Maafisa Ushirika ambao ndio wasimisizi wa karibu sana wa vyama hivyo.
"Pamoja na jitihada za Serikali katika kuendeleza kilimo chenye manufaa kwa wakulima na kusimamia vyama vya Ushirika ili viwasaidie wakulima bado kumekuwepo changamoto nyingi kwenye yama hivyo nyingi zinatokana na usimamizi usioridhisha hivyokupelekea mianya ya madhaifu mbalimbali hususan upotevu wa fedha na mali zingine za wanaushirika "Mkuu wa Mkoa anaeleza na kuongeza kuwa,
"Udhibiti na usimamizi katika vyama hivyo umekuwa mdogo kutokana na hawa ambao ndio wenye jukumu la kuvisimamia vyama hivyo katika maeneo yao kwa kila Wilaya kukosa ujuzi na uzoefu wa kusimamia kwa weledi unaotakiwa, mfano; vyama vya ushirika vinatakiwa kukaguliwa lakini vimekuwa havikaguliwi kikamilifu kutokana na Maafisa kukosa ujuzi wa ukaguzi, ujuzi huu unakosekana kwa sababu ya ukosefu wa mafunzo ya mara kwa mara kwa Maafisa hao hivyo mafunzo haya yajikite katika kutatua changamoto za kiujuzi na kiutendaji kwa Maafisa." anaeleza.
Anasema uwepo wa malalamiko mengi
kutoka kwa wakulima juu ya baadhi ya
Maafisa Ushirika kukiuka taratibu za utumishi wa Umma na kujiingiza katika
vitendo vya rushwa, usababishaji wa migogoro na kushirikiana na baadhi ya
watendaji wa Vyama vya Ushirika katika kuvihujumu Vyama hivyo anafurahi kusikia hatua za nidhamu zimekuwa zikichukuliwa kwa wote waliothibitika kufanya matendo hayo.
Kwa upande wake Dkt .Benson Ndiege ,Mrajis wa vyama vya ushirika na Mtendaji anaeleza tume ya maendeleo ya ushirika ni taasisi iliyopewa dhamana ya kusimamia maendeleo ya ushirika nchini na inasimamia sheria ya vyama vya ushirika ya mwaka 2013 namba 6 .
Anasema sheria inataja majukumu mawili ambayo ni uhamashishaji wa ushirika na udhibitisho ama usimamizi wa vyama vya ushirika ambapo katika eneo ambalo lina tatizo ni Udhibiti na usimamizi ambalo linahitaji uangalizi kwani utafiti walioufanya unaonyesha vyama vingi vya ushirika mwaka 2019 na 2020 asilimia 60 ndivyo vimeweza kukaguliwa na kusimamiwa ipasavyo vingine vyote asilimia 40 havikuweza kufikiwa ipasavyo.
" Tulijiuliza ni kwa nini ili lilitokea Utafiti wetu unaonyesha kuwa labda changamoto ipo kwa maafisa ushirika kwa sababu takwimu zinaonyesha asilimia zinaonyesha asilimia 33 ya maafisa hao ndio wenye uwezo wa kukagua kikamilifu vyama vya ushirika vya aina mbalimbali ili uweze kutoka kwenye hili dibwi lazima asilimia 100 ya maafisa ushirika wawe na huo uwezo hapo ndipo wataondokana na hilo tatizo la kutokagua vyama vya ushirika na kutovisimamia ipasavyo ."anaeleza
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ,Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara anasema unatambua umuhimu wa mafunzo hayo imani yao mafundisho waliyoyapata wataenda kufanya vizuri.
Alisema kuna mambo makubwa yanayofanyika mkoani humo ikiwemo ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ambalo limeanza kwa kasi kubwa hivyo tuendelee kuhamasisha vyama vya ushirika ili viweze kujiunga katika shughuli hiyo hadi sasa wanavyama 21 ambavyo vimejiunga na vimeomba mkopo wa billion 3.2 .
Hivyo aliwaomba na Maafisa ushirika ndani na nje ya Mkoa wanaoishi maeneo ya ziwa waweze kuhamasisha ufugaji huo .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.