MSINGI WA MALEZI BORA KWA MTOTO UNAJENGA TAIFA IMARA: RC MTANDA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Mei 21, 2025 amefungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa program jumuishi ya Taifa ya malezi na makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na kusisitiza Taifa lolote imara litatokana na msingi imara wa malezi bora ya mtoto.
Akizungumza na Maafisa Ustawi wa Jamii na Maafisha Lishe kutoka mikoa ya Bara na visiwani kwenye ukumbi wa Adden Palace wilayani Ilemela, Mtanda amesema mkakati wa kuwekeza malezi na makuzi kwa mtoto hauna budi kuwa endelevu ambao utaleta matokeo chanya kuwa na Taifa lililostaarabika.
"Niwapongeze Tamisemi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum kwa kuwa na mpango huu wa kufanya tatmnini kila robo mwaka hali ambayo inaongeza ufanisi kujua wapi kuna mafanikio na changamoto", Mkuu wa Mkoa.
Hali kadhalika, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha umri kuanzia 0 hadi 8 unaowalznga watoto hao ndiyo muhimu wa kuanza kumpa malezi na makuzi bora tofauti na umri huo ni tishio kwa ustawi wa Taifa.
Kwa upande wake mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum Bw. Sebastian Kitiku amesema tathmini wanayofanya imewashirikisha Maafisha Lishe pia ambao ni wadau wakubwa wa kuhakikisha afya bora ya mtoto.
"Mpango huu umeanza mwaka 2021 na ueizinduliwa na Mhe.Rais hadi sasa umekuwa na matokeo chanya kutokana na tatmninini hizi tunazofanya," Naibu Katibu Mkuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.