Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba kukagua ujenzi wa Hoteli ya Nyota Tano inayojengwa na Mfuko huo wa Hifadhi ya Jamii.
Akizungumza baada ya Ukaguzi huo Mhe. Mtanda amewapongeza NSSF kwa ukaguzi huo mkubwa na akatoa wito kwao kukamilisha ujenzi kwa viwango na kasi inayokusudiwa ili kufikia mwezi Julai 2026 wakamilishe.
Mhandisi Suleiman Salmin msimamizi wa Mradi huo amebainisha kuwa kazi zinazoendea kuwa ni pamoja na ukamilishaji wa mabwana ya kuogelea na urembo, ukamilishaji wa vyumba 185 vya kulala pamoja na urembo.
Awali, Mkuu wa Mkoa ameongoza kikao kati ya Mfuko wa hifadhi ya Jamii (NSSF) pamoja na Wilaya za Magu na Ilemela kufuatia migogoro ya Ardhi kwenye maeneo ya Kiseke na Kisesa (Kanyama) iliyosababishwa na Uvamizi wa wananchi kwenye maeneo ya hifadhi hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.