Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ametoa wito kwa Wanawake wamiliki wa Shule na Vyuo binafsi nchini, kuwekeza katika sekta ya elimu kupitia elimu ya amali hasa miundombinu iyakayosaidia kurahisisha utekelezaji wa mtaala mpya.
Prof. Mkenda ametoa wito huo leo Julai 23, 2025 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa nne wa Chama cha Wanawake Wamiliki wa shule na vyuo Binafsi Nchini, ambapo amewataka Wamiliki hao kushirikiana na serikali katika kutengeneza mkakati wa pamoja wa kuona namna gani wanavyoweza kufanikisha utekelezaji wa elimu ya amali.
“Njooni tuongee, mkitaka kujenga shule za amali, sports academy, njooni tuongee tuone tunawezaje kusaidia”.
Prof. Mkenda amesema dhamira ya serikali ni kuona wanafunzi wanaopatiwa ujuzi wanakuwa na ubora wa kimataifa ambapo itawasaidia kiweza kufanya kazi mahali popote pale duniani.
Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza ni Mkoa wa kimkakati hali iliyoipelekea Serikali ya awamu ya sita kuwewekeza zaidi ya shilingi bilioni 196 katika kujenga miundombinu na uratibu wa shughuli za elimu.
“miundombinu ya elimu imeboreshwa ambayo imesaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa umbali wa kutembea kwenda shule, msongamano wa wanafunzi madarasani, kuwezesha mazingira bora zaidi kwa walimu na wanafunzi”.
Elimu ya amali ni njia ya elimu inayolenga kuwafundisha vijana ujuzi wa vitendo unaohitajika moja kwa moja kwenye soko la ajira, kama umeme, ujenzi, utengenezaji, ufundi mbalimbali, TEHAMA, sanaa na kilimo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.