RAIS SAMIA ATOA ZAWADI KWA WAHITAJI MWANZA
Wananchi wameombwa kuendelea kuishi kwa kupendana na kujaliana na hasa kwa wale wenye mahitaji maalum ili wasione wametengwa na jamii.
Rai hiyo imetolewa leo Januari 31, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyetoa zawadi ya sikukuu kwenye vituo vya wenye mahitaji maalum kikiwemo chuo cha ufundi Mirongo- Nyamagana na kubainisha kuwa wenye mahitaji maalum pia wanamchango wa kujenga uchumi wa nchi hii, hivyo wajibu wetu ni kuwaonesha upendo na kuwajali.
"Nipo hapa kwa niaba ya Rais na salamu zake ziwafikie wote, hawa wenzetu wenye ulemavu mara baada ya kumaliza masomo yao hapa watakwenda kujenga uchumi wa Taifa letu, hatuna sababu yoyote ya kuwatenga zaidi ya kuendelea kuwatia moyo kama anavyoonesha mfano mzuri Rais wetu,"amesisitiza mkuu wa mkoa.
Mhe.Mtanda amesema zawadi hizo za sikukuu zimekwenda pia kwenye vituo vingine viwili, kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Imani kilichopo wilayani Misungwi na kituo cha Mavuno kilichopo wilayani Magu.
Zawadi hizo ni mchele,unga wa ngano,unga wa ugali,sukari,mafuta ya kupikia,mbuzi,mafuta ya kupaka,viungo vya kupikia na vinywaji baridi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.