RAIS SAMIA ATOA ZAWADI ZA SIKUKUU YA KRISMAS KWA WATOTO YATIMA NA WENYE MAHITAJI MAALUM MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amekabidhi zawadi za Sikukuu ya Krismas kwa niaba ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalum katika vituo vya malezi vya Tawfiq kilichopo Mhandu-Nyamagana na TCRC-Nyasaka Ilemela.
Akizungumza katika nyakati tofauti baada ya kukabidhi zawadi hizo Mhe. Mtanda amemshukuru Mhe. Rais kwa kuamua kusherehekea Sikukuu pamoja na watoto kwa kuwakumbuka kwa zawadi ili watoto hao wale na kunywa na kufurahia siku kuu hiyo.
"Kwa zawadi hizi namshukuru sana Mhe. Rais kwani watoto hawa leo watafurahia na kutambua kuwa wanao walezi pamoja na kwamba hawana wazazi, watakula na kunywa kwa furaha kwani amewakimbilia yatima na wajane hawa." Mhe. Mtanda.
Aidha, amebainisha kuwa serikali itaendelea kushirikiana na vituo vya malezi ya watoto wakati wote kwani lengo la wenye vituo ni jema na la kiutu sana hivyo ni lazima serikali iwaunge mkono.
"Watu wa Ustawi wa jamii endeleeni kusimamia vituo hivi na kuwapa miongozo ili wapatiwe elimu na kukomesha matendo ya ukatili wa watoto na kijinsia katika maeneo ya vituo vya malezi." Amesisitiza Mkuu wa Mkoa.
"Kituo hichi kinajumuisha watoto yatima na wenye wazazi lakini wanaotoka kwenye mazingira magumu, kimesajiriwa mwaka 2019 na kwa sasa kina watoto 25 na tunafuata miongozo kutoka kwa serikali ikiwemo kuwapatia Elimu." Salum Juma Khatib, Mkuu wa Kituo cha Tawfiq.
Pamoja na zawadi hizo za Maharage, Mbuzi, Mchele, Sukari, Sabuni za vipande na za unga, Mafuta ya kupikia, Soda, Juice ambavyo kwa pamoja vina thamani ya zaidi ya Tshs. Milioni 2, Mhe. Mkuu wa Mkoa binafsi amekichangia kituo cha Tawfiq Tshs. Milioni 1.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.