Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike amehimiza jitihaza za haraka zifanyike ili Vyuo vya Elimu ya Juu na Taasisi vilivyopo Mwanza vifahamike kwa Wananchi ili Wanafunzi kutoka ndani na nje ya Mkoa huo wapate nafasi ya kuja kusoma.
Katibu Tawala Ngusa amesema hayo juni 09, 2022 wakati wa ukaguzi wa Jengo jipya la Taasisi ya Uhasibu tawi la Mwanza linalojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 7.8 na akabainisha kuwa bado Wanafunzi wengi wanakwenda kusoma nje ya Mwanza wakati vipo hapa ni lazima kuwepo na mkakati wa kuvitangaza.
"Mwanza ni Mkoa wa Kimkakati na unazungukwa na Nchi za Maziwa Makuu,nawapongeza Taasisi ya Uhasibu kwa mpango huu nawaahidi kushirikiana nanyi ili tufikie malengo"
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania,Prof William Pallangyo amesema kwa sasa wana Matawi sita mpango uliopo ni kutanua zaidi.
"Taasisi yetu ni kongwe imeanza tangu miaka ya 1970 ikiwa inaitwa Chuo cha Uhasibu na sasa ni Taasisi ya Uhasibu ikiwa na jumla ya Wanafunzi 23620" Prof Pallangyo.
Taasisi ya Uhasibu Tanzania kwa sasa ina Matawi katika Mikoa ya Mwanza,Mtwara,Singida,Dsm,Mtwara, Mbeya na Kigoma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.