• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC. MAKALLA AITAKA HALMASHAURI YA SENGEREMA KUKARABATI BOTI YA WAGONJWA

Posted on: June 22nd, 2023

RC. MAKALLA AITAKA HALMASHAURI YA SENGEREMA KUKARABATI BOTI YA WAGONJWA


Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. CPA. Amos Makalla ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema kufanya tathmini ya kukarabati boti ya wagonjwa ambayo ni mali ya Halmashauri inayosafirisha wagonjwa kutoka katika kisiwa cha Juma.

Amesema hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa leo Juni 22, 2023 wakati wa Mkutano na Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) za Mwaka 2021/ 2022 katika Wilaya ya Sengerema.

"Hii boti siyo ya muda mrefu sana Halmashauri ikafanye tathmini ya ubovu wa hiyo boti na gharama za utengenezaji na kama gharama za ukarabati ni ndogo kuliko ya kununua mpya basi itengeneze kwa kuwa itawasaidia kuwafikisha kwa haraka wa mama wajawazito na watoto katika vituo vya vya kupatiwa huduma",amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa

"Hoja hii ya miradi ya zaidi ya Shilingi Milioni 202 ambayo haijakamilika katika ngazi za chini  inatakiwa iwe imekamilika ikifika mwisho wa mwezi huu na nitahitaji nipate taarifa ya hii miradi",Balandya

Aidha Ndg. Balandya ametoa rai kwa Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema ihakikishe kwamba utaratibu wa ununuzi unazingatiwa  kufuatia mapungufu yaliyobainika katika ununuzi na ufungaji wa taa za barabarani katika barabara yenye urefu wa kilomita 5.6 zenye thamani ya zaidi ya  shilingi Milioni  549.

Pia Ndg. Balandya amemtaka Mganga Mkuu wa wilaya ya sengerema Dkt. Fredrick Mugalura   kuhakikisha anafuatilia kibali kutoka TMDA cha kutekeketeza dawa zilizo china zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 42 ili kuepusha athari za matumizi ya dawa hizo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Sengerema Bw. Binuru Shekidele  amesema Halmashauri itawaita wananchi waliojenga vibanda vya biashara katika stendi ya Bukala na kuikosesha Halmashauri mapato ya Shilingi Milioni 61.2 ili kuweza kuiona  mikataba yao na kufikia makubaliano.

Mwakilishi wa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali Mkoa wa Mwanza Waziri Shabani amesema  kwa hesabu za mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya Sengerema ilipata hati inayoridhisha  kutoka kwa mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa hesabu za serikali.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema amesema kwa hoja ambazo zinahusu Halmashauri zifanyiwie mchakato wa haraka wa kuzimaliza ili ziweze kufungwa na kuipatia Halmashauri hati safi  ya udhibiti.

Sambamba na hayo Ndg. Balandya amewataka  Madiwani wa Wilaya ya Sengerema kuisimamia Halamashauri ili kuhakikisha mapungufu yanarekebishwa na miradi inatekelezwa kikamilifu na kuhakikisha wanawasimamia vijana wanao jiajiri  ili kuondoa umasikini katika wilaya hiyo.

Wilaya ya Sengerema Ina jumla ya Kata 26 na Tarafa 3.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.