RC MAKALLA AWASHANGAZA WANANCHI SENGEREMA ASIKILIZA KERO KUANZIA ASUBUHI MPAKA USIKU
*Mamia ya wananchi wasikilizwa na kutatuliwa kero*
*Wengi Wampongeza wawataka watendaji walio chini yake kumuiga*
*Aagiza watendaji vijiji, kata na idara kujipanga na kushughulikia kero zote za ardhi*
*Amesema utaratibu wa kushuka kwa wananchi ni wa kudumu*
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla ameendelea na ziara zake za kupita katika kila halmashauri kusikiliza na kutatua kero za wananchi na siku zingine kukagua miradi ya maendeleo.
Mkuu huyo wa mkoa yupo wilayani *Sengerema* kwa ziara ya siku tatu za kusikiliza kero na kukagua miradi ya Maendeleo.
Jana Novemba 08, 2023 wananchi wa Sengerema walifurika kwenye viwanja vya stendi ya zamani ya mabasi kuwasilisha kero ambapo Mhe. Makalla amesikiliza kero kuanzia asubuhi mpaka usiku.
Wananchi wa Sengerema wamefurahishwa sana na utaratibu wa Mkuu wa Mkoa na wamewataka watendaji wa chini kumuiga katika kutatua kero zao.
Mkuu wa Mkoa tayari ameshafanya ziara za usikilizaji kero na ukaguzi wa miradi kwenye wilaya za *Nyamagana*,*Ilemela* *Magu* *Misungwi* na sasa anaendelea na ziara wilaya ya Sengerema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.