Leo Oktoba 27, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amefanya mahojiano maalumu na kituo cha televisheni Clouds ambapo amezungumza mambo mbalimbali yahusuyo Mkoa wa Mwanza.

Katika Mahojiano hayo RC Mtanda amezungumzia fursa za miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza kama vile ujenzi wa daraja la JP Magufuli, Meli ya Mv. Mwanza Hapa kazi tu, Ujenzi wa Masoko makubwa Jijini Mwanza na Ilemela Manispaa, Upanuzi wa uwanja wa ndege Mwanza, Huduma za Afya, Elimu, Maji, Umeme n.k

Aidha amezungumzia pia kuhusu maandalizi ya uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano Oktoba 29, 2025 ambapo amesema katika Mkoa wa Mwanza wamejipanga kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.