RC MTANDA AFUTURISHA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Serikali itaendelea kuweka mikakati ya kuwapatia stadi za maisha ili kusaidia kuwaondoa watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi mtaani na kuhakikisha wanakua na shughuli rasmi za kujipatia kipato.
Ametoa kauli hiyo jioni ya leo Jumatano Machi 12, 2025 wakati wa hafla ya kufuturisha aliyoiandaa kwa kundi hilo iliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambayo imewakutanisha zaidi ya watoto 300 kutoka katika viunga mbalimbali vya Jiji hilo
Mhe. Mtanda amebainisha kuwa kuanzishwa kwa vyuo vya mafunzo stadi kupitia VETA ni moja ya juhudi hizo ambapo vijana kuanzia darasa la saba wanapokelewa na kupewa ujuzi wa fani mbalimbali ili kusaidia kila kijana awe na kazi ya kufanya.
"Nataka kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuhangaika na watoto wa mtaani kwani tukiwaacha kundi kubwa hivi ni kupoteza nguvu kazi ya Taifa ambayo madhara yake ni makubwa kwa siku za usoni." Amesema Mhe. Mtanda.
Aidha, ametoa wito kwa Maafisa Ustawi wa jamii kuendelea na juhudi za kuwafikia makundi mbalimbali ya wahitaji na kuwapa mwanga na muelekeo wasije wakaingia kwenye kazi hatarishi kama kuvuta bangi na kunywa pombe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.