• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

RC MTANDA AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA KUONGOZA KUPATA FAIDA

Posted on: January 30th, 2025

RC MTANDA AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA KUONGOZA KUPATA FAIDA


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amefanya mazungumzo na Meneja mpya wa Kanda ya ziwa kutoka benki ya NMB Bi. Faraja Ngingo

na kuipongeza Taasisi hiyo kwa kuwa kinara wa kupata faida nchini ya shs bilioni 644 baada ya kukatwa kodi.

Akizungumza na mgeni huo ofisini kwake leo tarehe 30 januari, 2025 Mtanda amebainisha kuwa kufanya vizuri kwa taasisi hiyo kunazidi kuwapa imani wateja wake na kupiga hatua kiuchumi.

"Hongereni sana natambua Serikali nayo ina hisa ya 31% mkakati yenu ya kuinua uchumi wa Taifa ni mizuri ikiwemo utoaji wa mitaji mikubwa ya mikopo kwa wafanyabiashara huku mkiwa wabunifu kwa wafanyabiashara wadogo na Ile mikopo isiyolipika ikishuka kwa asilimia 2.9,ni dhahiri NMB ni benki ya mfano wa kuigwa," Mtanda.

Aidha ametoa ushauri kwa benki hiyo kuzidi kutanua wigo wa ubunifu wa kulisaidia kundi kubwa la vijana kwa kuwaongezea mitaji ya mikopo hasa kutokana na fursa zinazoanza kuja mkoani Mwanza mara baada ya miradi ya kimkakati kukamilika

"Kwa mwaka huu tumetenga shs bilioni 6.4 ambazo zitakwenda kusaidia shughuli za afya na elimu huku tukiendelea na mpango wetu wa kuwadhamini wanafunzi 65 kila mwaka waliopata ufaulu wa daraja la juu na wanaotoka kwenye kaya masikini kwa masomo  ya elimu ya juu," Bi.Faraja.

Amesema mara baada ya mkutano wa kimataifa wa wadau wa nishati ya umeme kumalizika Jijini Dar-e-s-Samaam,benki ya NMB kwa kutambua mnyoroeo wa thamani kwenye eneo hilo, imetenga shs bilioni 100 na itatoa mkopo wa shs bilioni 1 kwa mtu watakao jishughulisha na nishati ikiwemo na uuzaji wa gesi.

Benki ya NMB mwaka 2024 imepata faida ya shs bilioni 931 na baada ya makato ya kodi imepata shs bilioni 644.

Wakati huo huo uongozi wa benki ya maendeleo ya kilimo TADB Kanda ya ziwa umesema mwaka 2024 umetoa mkopo wenye thamani ya shs bilioni 38 kwa makundi ya kilimo cha mazao,mifugo na uvuvi

Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza aliyefika Ofisini kwake kutoa salamu za mwaka mpya,Meneja wa benki hiyo Alphonce Mokoki amesema upande wa uvuvi vi wametoa boti 55 zenye thamani ya shs bilioni 2.5 na vizimba 222 vilivyogharimu shs bilioni 6.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.