RC MTANDA AKABIDHI MAGARI MAWILI KWA MA-DC UKEREWE NA MAGU
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 23 Mei, 2025 amekabidhi magari mapya mawili aina ya “Land Cruiser Prado All Rounder Plus” kwa ajili ya Wahe. Wakuu wa Wilaya za Ukerewe na Magu na kutoa rai kuwa magari hayo yakatumike kama ilivyokusudiwa.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mtanda amesema kila gari moja limenunuliwa kwa Tsh. 252,384,800/= Hivyo ni jukumu la Wahe. Wakuu wa Wilaya hao kwenda kuyatunza vema.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wahe. Wakuu wa Wilaya hao wameishukuru Serikali kwa kupatiwa magari ambayo yatawawezesha kufika katika maeneo yao ya utawala kwa haraka na kuwahudumia wananchi.
“Tunaahidi kuwa tutayatumia magari haya kama yalivyokusudiwa na tutasimamia kuhakikisha yanatunzwa na kutumika kwa shughuli za Serikali katika kuwahudumia wananchi na kuahidi kuyatunza ili yaweze kudumu muda mrefu”. Mhe. Joshua Nassari Mkuu wa Wilaya ya Magu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.