Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema anamkumbuka marehemu Agnes Magupu aliyekuwa Afisa Michezo, Sanaa na Utamaduni kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza kama mtu aliyependa kazi yake na mwenye kujituma.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo Julai 2, 2025 alipowasili katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ambapo amesema anaamini Jiji la Mwanza wamepoteza mtu muhimu sana.
Mkuu wa Mkoa amesema alimtambua marehemu Agnes kupitia kujituma kwake, kujitoa na kufanya kazi kwa moyo, mchango na uwepo wake katika maandalizi ya shughuli mbalimbali za Serikali na mara ya mwisho alikuwa miongoni mwa Viongozi wa kamati ya maandalizi ya ziara ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Lakini wakati fulani nilikuwa na ziara ya kuwatembelea Viongozi wa dini hapa Mkoani Mwanza nikashangaa naenda ofisi ya Askofu mmoja nikamkuta pale na yeye akisema ni miongoni mwa Viongozi wa kanisa lile.”
“Kwa hiyo hii pia inamaanisha alikua mnyenyekevu hata kwa Mungu, sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejea Amina.” Amesema Mkuu wa Mkoa.
Marehemu Agnes Magubu amefariki dunia juni 30, 2025 akiwa njiani kutokea Mkoani Iringa katika ziara ya kikazi kushiriki mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA na ibada ya kumuaga itakua siku ya Alhamis Julai 3, 2025 katika kanisa la Kuu la Anglikana DVN – Kamanga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.