Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka Sekretarieti ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) kutatua migogoro yao kupitia vikao ili kuboresha zaidi mashindano hayo.
Mhe. Mtanda ametoa wito huo leo Septemba 16, 2025 katika uwanja wa Mpira wa CCM Kirumba wilayani Ilemela alipokua akifunga rasmi mashindayo hayo mwaka 2025 yaliyodumu kwa takribani siku 16 za mitanange kupitia michezo mbalimbali.
Amesema, wanapohitimisha michezo hiyo wahakikishe wanaketi pamoja na kushughulikia mapungufu yaliyojitokeza na kuyatatua ili kwenye michuano ijayo kuwe na ufanisi zaidi badala ya kukutana wakiwa na migogoro ambayo huathiri michezo.
Aidha, amewataka watumishi mbalimbali kujisajiri kwenye mfumo rasmi wa wanamichezo chini ya usimamizi wa sekretarieti ya SHIMIWI ili kuwa na kanzifata maalumu ya wanamishezo na kuweza kuhuisha kila wakati vinapotokea vipaji.
Vilevile, ametoa wito kwa shirikisho hilo kuhakikisha wanahusisha watu wenye ulemavu ambao wapo kwenye utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria na kushirkiana na wizara mama ya michezo katika kulinda na kuboresha miundombinu ya michezo.
Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Savera Slavatory ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa wizara hiyo amesema wanamichezo 3165 wameshiriki mashindano hayo kutoka kwenye vilabu 65 kwa muda wa siku 16 kwa mafanikio makubwa.
Aidha, ameahidi kuwa wizara hiyo itasimamia haki wakati wote kwa kuhakikisha sheria zinafuatwa na ameitaka sekretarieti ya SHIMIWI kurekebisha makosa madogo yaliyojitokeza kwa ajili ya kujifunza kwa michuano ijayo na akatoa rai kwa waajiri kuhakikisha wanapeleka watumishi kwenye michuano hiyo.
Awali uwanjani hapo, Mkuu wa Mkoa ameshuhudia fainali kwa michezo ya kuvuta Kamba ambapo Ofisi ya RAS Tanga wamewabwaga TAKUKURU kwa Wanawake huku OR- IKULU wamewapiga TAKUKURU wanaume. Na Mshindi wa jumla SHIMIWI 2025 ni TAKUKURU.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.