RC MTANDA AWATAKA VIONGOZI WA DINI NA WAUMINI KUIENZI NA KUENDELEZA AMANI
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka viongozi na waumini wa dini mbalimbali katika Mkoa wa Mwanza na Tanzania kiujumla kuendelea kuitunza na kuienzi amani ya nchi tuliyonayo kwani ndio tunu kwa Taifa letu.
Mhe. Mtanda ametoa rai hiyo alipokuwa akuzungumza katika muhadhara wa kongamanio la nasaha na dua lilioandaliwa na Alhadji shekhe Dkt. Seif Hassan Sulle katika Viwanja vya Furahisha Wilayanj Ilemela, ambalo limelenga kutoa elimu na nasaha kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo dini ya kiislamu na jamii kiujumla.
"Amani yoyote katika nchi yoyote inajengwa kwa misingi imara na kwa msiingi thabiti hivyo hata hapa kwetu kuna misingi thabiti iliyojengwa hivyo lazima tuienzi na tuikumbatie amani yetu,"Mtanda
Tunajua amani yetu ndio tunu yetu na wale wanaofanya kazi iyo lazima watiwe moyo, waungwe mkono wasaidiwe ili waweze kufikia malengo ya kuhakikisha amani yetu inadumu. Amesema Mkuu huyo wa Mkoa.
Aidha Mhe. Mtanda pia amesema endapo katika jamii zetu kutatokea kuitilafiana au kutokuelewana basi hakuna budi kuandikishana mikataba ya amani ambayo itatusaidia kuishi katika misingi ya kupendana na kuheshimiana.
Naye Shekhe Dkt. Sulle amesema muhadhara huo umelenga kutoa elimu kwa waumini wa dini zote kuhusu thamani ya ya amani na nchi waliyonayo lakini pia kufanya dua maalumu ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda pamoja na viongozi mbalimbali wa Kitaifa.
"Ni wajibu wetu sisi kama waamini kumuombea Rais wetu na viongozi wetu na wao ni binadamu wa kawaida, nguvu yao ni dua, tukiwafanyia dua wanakua imara". Shekhe Dkt. Sulle.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.