Taasisi ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na Serikali imeahidi kuendelea kutoa huduma za afya, kujenga vyumba vya upasuaji na kujenga nyumba za watumishi wa afya katika maeneo mbalimbali nchini ili kuboresha mifumo na huduma bora za afya kwa jamii.
Akiongea katika warsha ya ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii yatakayodumu kwa siku mbili jijini mwanza, Afisa sera na uraghabishi Bi. Christina Godfrey alisema, mafunzo hayo yatawawezesha wahudumu hao kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo tarajia katika jamii.
“ Matarajio ya mafunzo haya ni kutoka na mkakati utakao wahusisha viongozi wa jamii,namna ya kutatua changamoto zitakazo ibuka baada ya kuwaweka wahudumu katika ngazi ya jamii na njia watakazo tumia katika kutatua changamoto hizo katika halmashauri zao” alisema Godfrey.
Naye Mratibu wa huduma za afya ngazi ya jamii Dokta Shaba Kelasi alisema kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa muda wa mwaka mmoja ili kuwajengea uwezo wahudumu wa afya kutoa huduma hizo katika vipengele tofauti tofauti kama programu ya mama na mtoto ,ukusanyaji taarifa, ukimwi, lishe,uzazi wa mpango, takwimu na magonjwa ya mlipuko kwa wakati mmoja.
“ Mafunzo haya yanatolewa kwa mwaka mmoja kwa lengo la kuwawezesha wahudumu wa afya ili kuwabadilisha wale wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao walikuwa wakifundishwa kwa muda mfupi ili wawe na uwezo mkubwa wa kutoa huduma za jamii ukilinganisha na wale wanaosoma programu husika” alisema Kelasi.
Akimuwakilisha Mganga mkuu wa Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa, Dokta Sailas Wambura alisema, mafunzo hayo yatasaidia kupunguza ongezeko la maambukizi ya virusi vya Ukimwi na vifo vya mama na mtoto suala ambalo limekuwa changamoto kwa Mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.