• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Tanzania Tumejaaliwa utajiri wa asili - Waziri Kigwangala

Posted on: July 4th, 2019


Waziri wa  Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala amesema  Tanzania itakuwa moja ya taifa tajiri endapo itachukua hatua madhubuti ya kuhifadhi  maliasili  zilizopo kwa sasa.

Dk. Kigwangala amesema Tanzania ndani ya miaka 10 ijayo watanzania watakadiriwa kufikia milioni 100 na baada ya miaka 100  watafikia milioni 200, hivyo kutakuwa na changamoto kubwa  ya mahitaji ya binadamu  kama maji, umeme, ardhi, chakula na hewa.

Alisema endapo hatua za uhifadhi  wa maliasili zitachukuliwa mapema, Tanzania itakuwa tajiri na taifa lenye usalama zaidi  kutokana na kuwa na hifadhi za taifa,  maziwa, mito na ardhi ya kutosha tofauti na mataifa mengine hivyo  watanzania watakuwa na uwezo  kuendesha kilimo cha umwagiliaji kwa misimu mitatu kwa mwaka.

“Tanzania ni moja ya nchi iliyo tofauti na mataifa mengine, imejaliwa na kuwa na maliasili na vivutio kadhaa ambavyo hata nchi nyingine  hazitapata tulichonacho, naomba niwaambie hifadhi ni utajiri mkubwa sana.

“Nasema hivyo kwa sababu  idadi ya watu inaongezeka  kila siku tena kwa kasi kubwa lakini vile vitu tunavyohitaji ili tuishi ni vile vile na tusipovitunza kizazi kijacho cha  watanzania wa miaka 50 ijayo  kitakadirikiwa  kufikia milioni 100, baada ya miaka 100 tena tutafikia milioni 200 hebu tujitafakari hapo mahitaji yatakuaje.

“Mahitaji yatakuwa makubwa kuazia maji, umeme, chakula , hewa na vitu vingine na kama Tanzania tutachukua hatua mapema  ya kulinda rasilimali zilizopo  tutakuwa na  taifa tajiri kwa sababu tuna maji ya baridi tunayo ambayo pengine watanzania wanaweza kufanya shughuli za kilimo  cha umwagiliaji mara tatu kwa mwaka na kuachana na kutegemea mvua.

“Leo baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kulalamika kukosa chakula na mmeona juzi juzi Mhe. Rais Dkt.John Magufuli ametembelea baadhi ya mataifa ikiwamo Zimbabwe wametuomba chakula na tumetoa, Tanzania tuna vitu vya kipeke kama hifadhi ya Serengeti ambayo nchi nyingine hazina, hivyo vitu kama hivi lazima tutunze, huwezi kuamini Ziwa Manyara linaweza kutoweka kutokana na kina chake kupungua, leo ukiambiwa Sinza au Magomeni pale Dar es Salaam kulikuwa na  bwawa huwezi kuamini,”alisema.

Dk. Kigwagala alisema hapo mbeleni kutakuwa na shida ya maji sana na wabunge wa miaka 50 au 100 ijayo watakuwa wanadaiwa na wananchi wake kupelekewa huduma ya maji ya bomba kwa ajili ya kilimo na si matumizi ya nyumbani kama ilivyo sasa.

Tanzania  kwa miaka hiyo itakuwa tajiri  kutokana na kuwa na ardhi na maji ya baridi ambapo  kuna uwezekano wa kuwa na  maghala ya chakula kwa ajili ya kuzihudumia nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Aliongeza kuwa hivi sasa  Serikali imekusudia kujenga  kivuko cha watalii wa majini ambapo kitafanya shughhuli ya kutembelea hifadhi ya kisiwa cha Saanane,  Chato, Lubondo na hifadhi zingine zilizo pembezoni mwa ziwa Viktoria.

Alisema  sekta ya utalii ndio inaongoza kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia tano, hivyo ni dhahiri inapaswa kutunza kikamilifu.

Naye  Kamishna wa Tanapa, Allan Kijazi alisema hifadhi za taifa zilizopo kaskazini ndio zinaongoza  kutembelewa na watalii  tofauti na kanda zingine ambapo kama Serikali imejapanga kufanya mageuzi ili hifadhi zingine ziweza kufahamika zaidi na kutembelewa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella alisema mkoa huo ni kitovu cha nchi za Afrika Mashariki na ndio njia  ya karibu kwenda hifadhi ya Serengeti ambapo aliongeza kuwa kisiwa cha Saanane  ambacho ni pekee kutokana na kuwa ndani ya Ziwa Viktoria na Jiji la Mwanza.

Hata hivyo aliziomba wizara nyingine kutembelea mikaoni na kutoa mikakati yao ili viongozi wa mikoa waweze kujua  cha kufanya  wakati wakitimiza wajibu wao.

Akitoa neno  la shukrani kwa niaba ya wahariri wenzake, Abdallah  Majura, alisema  semina hiyo kwa wahariri na waandishi waandamizi itawaongezea maarifa mapya juu ya masuala ya Tanapa huku akimpongeza Dk. Kigwangala namna alivyoongoza wizara hiyo na kuleta mafanikio chanya kwa muda mfupi.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.