• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

TCCIA Yaiomba Serikali kufanya uwekezaji wa Kimataifa viwanja vya Nyamuhongolo

Posted on: August 18th, 2019


CHEMBA  ya Wafanyabiashara,wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) imeiomba Serikali kuipatia  eneo la Nyamhongolo jijini Mwanza ambalo limekuwa likitumika katika maonyesho ya  wakulima maarufu nane nane ili kuliwekeza katika hadhi ya kimataifa.

Ombi hilo lilitolewa  na Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mwanza, Dkt. Elibariki Mmari wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya ufunguzi wa maonyesho ya  14 ya Afrika Mashariki   yanayotarajiwa kuzinduliwa Agosti 30, mwaka huu na Waziri  wa Viwanda na Biashara,Mhe. Innocebt Bashungwa.

Dkt. Mmari amesema  maonyesho hayo  yanafanyika katika viwanja vya jengo la Biashara la Kimataifa la Rocky City Mall jijini Mwanza ambapo nchi za Kenya, Uganda,Rwanda, Indonesia, India, Syria, China na kampuni 300  zimethibitisha kushiriki.

Ameongeza kuwa TCCIA imekuwa katika changamoto ya muda mrefu ya kupata eneo la kudumu la  uwekezaji  kwa ajili ya maonyesho hayo ambapo ilifanya mazungumzo  ya awali na uongozi wa Mkoa wa Mwanza lakini walishindwa kufikia muafaka kuwapo na mpango wa maonyesho ya nanenane kikanda.

“Kama Serikali itatupatia pale Nyamhongolo tuna uwezo wa kujenga majengo yenye hadhi ya kimataifa na shughuli zitakuwa zikifanyika kwa mwaka mzima badala ya kusuburia nanenane, tutakachofanya   ni kuzingatia mahitaji  makundi yote ambapo  wale watakaokuwa wanahitaji eneo ni kulipia kama kawaida.

“Awali tulifanya mazungumzo na viongozi wa mkoa lakini kukawa na taarifa ya maonyesho ya nanenane yanatakiwa kuhamia Mwanza ambapo mpango huo ulishindikana na kuwapo mgawanyo, sote ni mashahidi wengine wanafanyia Simiyu, mikoa mingine hapa Mwanza.

“Bado tunafuatilia suala hili lakini tunaiomba Serikali itupatie lile eneo ili tulifanyie uwekezaji mkubwa na kuwa na hadhi ya kimataifa ili mataifa yanayohudhuria maeonyesho yetu yawe na uhalisia wa kile tunachokifanya, kwanza mapato ya nchi yatapatikana kwa urahisi na shughuli zitakuwa zikifanyika muda wote wa mwaka kama ilivyo Rocky City Mall,”alisema.

Dkt. Mmari alisema maonyesho ya mwaka huu yatakuwa tofauti na miaka mingine kutokana na mataifa makubwa  nje ya Afrika Mashariki kushiriki ambapo mapungufu yote yaliyojitokeza mwaka jana yamefanyiwa kazi huku akiwataka wananchi kujitokeza kutembelea kwani kutakuwapo na wanyama wakiwamo simba, fisi,chui, ngamia na wengine ambao watapata fursa ya kuwaona na kupiga picha.

Dkt. Mmari alisema miongoni mwa fursa zitakazopatikana kutokana na maonyesho hayo ni kuimarisha mtandao wa masoko na usambazaji bidhaa,  kampuni za Tanzania kujifunza na kutanua wigo wa biashara kwa kutumia makubaliano ya kibiashara ya kimataifa.

Vile vile alisema kufanyika maonyesho hayo yanatoa mchango kwa vitendo katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Magufuli kuifanya Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati ifikipo 2025 sambamba na kuimarisha mtengamano wa soko la pamoja la Afrika Mashariki.

Hata hivyo alipiga marufuku baadhi ya bidhaa zikiwamo silaha za moto na milipuko, masuala ya siasa na dini hayaruhusiwi katika maonyesho hayo huku akiwataka kampuni na watu binafsi wanaotaka kuwa wadhamini katika shughuli hiyo kujitokeza kabla ya Agosti 25, mwaka huu.

Alisema maonyesho hayo yatakuwa na zawadi kwa washindi katika makundi mbalimbali yakiwamo   wahandisi,  kilimo, viwanda, chakula, dawa na makundi maalum ambapo aliwataka washiriki kutambua jopo la majaji litaanza kupita kwenye mabanda yao kuanzia Agosti 31 hadi Septemba Mosi mwaka huu.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.