TUMIENI ELIMU HII KUSTAWISHA USHINDANI WA HAKI NA KUMLINDA MLAJI KATIKA SOKO: RAS Balandya
Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Rasilimali watu na Utawala Daniel Machunda leo Aprili 15, 2024 amefungua semina ya elimu kwa wadau wa Baraza la Ushindani na kuwataka kulitumia jukwaa hilo ili kustawisha ushindani wa haki na kumlinda mlaji katika soko.
Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Machunda amebainisha Baraza hilo ni muhimu kwa wadau hao ili kupata uelewa wa kutosha na kutatua changamoto zinazohusu ushindani wa kibiashara na udhibiti wa soko.
"Ndugu wadau Baraza la ushindani ni chombo muhimu katika uchumi wa soko kwa utoaji haki kwa wote, kupitia elimu hii itatusaidia kuongeza kasi ya uwajibikaji katika soko,"amesema Machunda.
Mkuu wa Idara ya uchumi kutoka Baraza hilo Kulwa Msogoti amesema jukumu kubwa la chombo hicho ni kutoa maamuzi ya rufaa yanayotokana na maamuzi yanayotolewa na baadhi ya Taasisi ikiwemo Tume ya Ushindani FCC,Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati EWURA, na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu LATRA.
Baraza la Ushindani,Fair Competition Tribunal- FCT ni Taasisi ya Serikali iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Ushindani Na. 8 ya mwaka 2003.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.