TUMIENI MAFUNZO MLIOPEWA KUWA WATUMISHI HODARI NA WENYE WELEDI:RAS BALANDYA
Watumishi wapya katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wameaswa kutumia mafunzo elekezi waliopewa kuweza kuwajenga kuwa watumishi hodari wenye weledi na kuwa tija kwa umma.
Rai hiyo imetolewa Aprili 18,2024 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa alipokuwa akizungumza na watumishi wapya mkoani humo katika ufunguzi wa mafunzo elekezi ya siku tatu yenye lengo la kuboresha utendaji wao wa kazi.
“Nawapongeza kwa kufanikiwa kuajiriwa katika Serikali ya awamu ya sita rai yangu kwenu tukaitumie vizuri nafasi hii ili thamani ya kuajiriwa iweze kuonekana kwa waajiri wetu na wananchi.”amesisitiza Mtendaji huyo wa Mkoa.
Naye Katibu Tawala Msaidizi Rasilimali watu na Utawala Bw. Daniel Machunda amemshukuru Katibu Tawala kwa kuridhia kuruhusu mafunzo hayo kufanyika na amewaasa watumishi wapya kuleta matokeo chanya katika majukumu waliopangiwa.
“Nakushukuru sana na kukupongeza ndugu Balandya umekuwa msaada sana mambo ya watumishi umekuwa ukiyapa kipaumbele”Daniel Machunda.
Kikao hicho kimehudhuliwa na watumishi 12 ambao wanatoka kada mbalimbali za utumishi ambao ni mkadiliaji majengo mmoja, madereva kumi na mtunza kumbukumbu mmoja.
Wakati huo huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndg.Balandya Elikana amekutana na kufanya mazungumzo mafupi Ofisini kwake na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Haji Janabi aliyeambatana na viongozi wengine waandamizi kwa ajili ya maandalizi ya kongamano la kukusanya maoni ya wadau kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya sera ya mambo ya nje ya mwaka 2001litakalofanyika Aprili 19,2024 Gold Crest Hotel.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.