Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana amewataka watumishi mkoani humo kuwa wabunifu kwenye kazi bila kusubiri kuelekezwa kutoka kwa wakuu wa idara na viongozi wao juu ya nini cha kufanya ili kuweza kupata matokeo mazuri

Ametoa wito huo kupitia kikao alichokifanya leo Disemba 2, 2025 na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambacho kilikua na lengo la kukumbushana majukumu ya kazi .

Aidha Ndg. Balandya amesema katika kufanikisha hilo watumishi katika idara zao wanatakiwa kushirikiana na kufanya kazi kwa ubunifu na ueledi ili kuunganisha taasisi nzima katika kuleta tija kwenye utendaji na kwa wananchi.

“Tuwe wabunifu kwenye kazi tutekeleze majukumu yetu yaliyo kwenye muundo wa ajira zetu kwani kila mmoja kwenye eneo lake anamuongozo wa majukumu ya msingi ya kufanya”. Amesema Ndg. Balandya.

Aidha, ametoa rai kwa watumishi kwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia kwa kuhakikisha wanaifahamu mifumo mbali mbali ambayo imewekwa ili kusaidia uharakishaji na ufanisi wa majukumu katika ofisi.

Akihitimisha kikao chake na watumishi Ndg. Balandya amewasihi kuilinda amani ya nchi na kuchukua tahadhari kwenye makazi yao wanapoishi.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.