Wamiliki na walimu wa shule za binafsi wametakiwa kufuata sheria ya uajili kwa kutoajiri vishoka na walimu kutoka nchi jirani bila vibali.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la Kitaalama la Kitaifa la Walimu wa Shule zisizokuwa za Kiserikali nchini Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Avemaria Semakafu kwa niaba ya Waziri wa Elimu Mhe. Prof.Joyce Ndalichako alisema walimu wa shule za binafsi wnaficha maovu ikiwemo suala la wizi wa mitihani.
"Maovu makubwa yanafanyika katika shule binafsi ambayo watekelezaji wake ni nyinyi walimu, unakuta mwalimu anafundisha siyo raia wa Tanzania na hana vibali lakini tukijua mnawatetea," alisema Semakafu.
Semakafu ameongeza kuwa Wizara yake isingetaka kuona Elimu yetu inayumba nchini.
Naye Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mwanza anayehusika na Masuala ya Elimu Michael Ligola aliwasisitiza walimu wafuate taratibu, kanuni na sheria zote ili kuhakikisha wanatenda haki.
"Malanyingi tumepata malalamiko hasa Shule binafsi kuwa wanaenda kinyume na taratibu zilizowekwa ikiwemo ukaririshwaji wa wanafunzi, "alisema Ligola.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa sheria mwenye uwezo wa kukaririsha wanafunzi ni kamshina Mkuu.
"Endapo itagundulika kuwa kuna shule iwe ya Serikali au Taasisi inakaririsha mwanafunzi kisa hajatimiza kigezo cha kuingia kidato kingine bila kibali cha Kamishina hakika tutachukua hatua,"alisema Ligola.
Naye Bwana Julius Mabula Katibu Mkuu wa Chama cha walimu shule binafsi Tanzania alisema, wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya waajili kutofuata sheria na taratibu ikiwemo kutishia au kuwafukuza kazi wakijiunga na chama chao.
"Waajiri wamekuwa wakiachishwa kazi walimu wanaojiunga kwenye chama chetu tukifuatilia tunaambiwa mwalimu kaondolewa kwa kukosa sifa," alisema Mabula.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.