• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Washauri wa Baraza la Nyumba na Ardhi waapishwa Mwanza

Posted on: August 20th, 2021

Washauri wa baraza ardhi na nyumba wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ,kuepuka vishawishi vya rushwa ,kufuata kanuni taratibu na sheria za ardhi ili kujenga imani kwa jamii.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Mhandisi Robert Gabriel mara baada ya kuapisha washauri wa baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya Sengerema alisema idadi ya migogoro inayotokana na matumizi ya ardhi imeendelea kuongezeka siku hadi siku.


Hivyo baraza hilo litapokea na kutatua migogoro itokanayo na matumizi ya ardhi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Buchosa mbayo inatatuliwa  kwa uharaka  na kuhakikisha haki inapatikana ili kuchochea maendeleo kwa wananchi.


Amesema awali wananchi walikuwa wakienda kupata huduma katika baraza la Geita ,kwa sasa watapata kwa urahisi hivyo viongozi waepukane na vishawishi vya  rushwa  watumie uzalendo na kuwa sababu ya faraja na utatuzi na kutokuwa chanzo cha migogoro.


" Mkoa unajukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora inayotolewa kwa ueledi na uadilifu hivyo utatuzi wa migogoro itokanayo na matumizi ya ardhi mhakikishe mashauri yanasikiliza na kuisha katika kipindi kisichozidi miaka miwili tangu shauri kufunguliwa katika baraza" alieleza Mkuu wa Mkoa.


Pia amezitaka alimashauri zote mkoani humo kuhuisha mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji kwa yale yaliyomaliza muda wake kutoa elimu kwa wajumbe wa mabaraza hayo ili kuboresha utoaji wa huduma pia wananchi watumie huduma hizo kikamilifu kupata ufumbuzi wa migogoro yao kwa mujibu washeria.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Senyi Ngaga alisema kati ya wananchi 100 anaowasikiliza asilimia 85 hadi 90 wote wanalalamikia migogoro ya ardhi hivyo baraza hilo litageuka chachu ya kupunguza migogoro hiyo pia kuwapumguzia wananchi umbali mrefu wa kufuata huduma hiyo mkoani Geita.


Naye Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Hamis  Tabasamu amesema kipindi cha Mhe.  kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana alikutana na malalamiko ya wananchi kutembea umbali mrefu  kutafuta haki kwenye baraza la ardhi Wilaya ya Geita,kuwapo kero hiyo na malalamiko mengi aliamua kutafuta ofisi ya kwa ajili ya baraza hilo kufanyia kazi zao.


"Kwa kushirikiana na Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema tukaamua ofisi ya mtendaji wa tuifanyie  marekebisho ili itumike kama ofisi ya Baraza la Ardhi la Wilaya ya Sengerema, Jumatatu ya wiki ijayo  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza atakuja kulifungua,'' alisema

Akiwaapisha wajumbe hao, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel alizitaka halmashauri zote mkoani humo kuhuisha mabaraza ya ardhi ya kata na vijiji.


Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.