Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amesema kufuatia Kampeni maalum aliyoiweka aprili 25 mwaka huu ya kurejesha fedha zilizokopwa na vikundi mbalimbali mkoani hapo na kutorejeshwa kwa wakati zaidi ya Tshs Bilioni 1.4 zirejeshwa serikalini .
Mhandisi Gabriel amesema hayo leo Julai 18, 2022 katika mkutano wake na waandishi wa Habari, ameeleza kuwa Tshs Bilioni 4.9 zilikopeshwa kwa vikundi mbalimbali katika kipindi cha Miaka mitatu ambapo hazikurejeshwa kwa wakati ndipo akawiwa kuanzisha kampeni ya kurudisha fedha hizo.
Vilevile, Mhandisi Gabriel amebainishaa kuwa mpaka sasa tayari Halmashauri za Mkoa huo zina Takribani Tshs. Bilioni 2.3 kwa ajili ya kukopesha kwenye vikundi vitakavyokidhi vigezo ametumia wasaa huo kuwakaribisha wananchi kuchangamkia fursa hiyo kuboresha mitaji yao.
Hata hivyo, Mhe. Gabriel ametoa wito kwa Maafisa Maendeleo ya jamii kutoka kwenye Halmashauri zote Mkoani humo kuvijengea uwezo vikundi kwa kuvipatia Elimu ya namna ya kuendesha miradi yenye tija na kuweza kurudisha fedha kwa wakati uliopangwa.
Aidha, Mhe Mkuu wa Mkoa amekemea suala la watumishi kuchukua fedha hizo kinyume na taratibu za fedha kwani kuna sheria na miongozo ya matumizi ya fedha hizo kutoka kwenye kifungu cha Maendeleo kutokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halamshauri.
"Sisi kama Serikali hatutalifumbia macho suala la watumishi wa umma kuchukua fedha zilizolengwa kwa vikundi na kujinufaisha wenyewe hivyo watumishi watakao husika tutawachukuli hatua", amesema Gabriel.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.