Aga khan Development Network kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada (Global Affairs Canada) kupitia mradi wa Improving Access to Reproductive Maternal and Newborn Health (IMPACT)Mwanza watoa vifaa kinga vya maambukizi ya Corona vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 20.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Emmanuel Tutuba alitoa shukrani kwa wadau wote waliguswa na kutoa misaada hiyo, aliahidi vifaa hivyo watavielekeza mahali palipokusudiwa pia aliwataka kutochoka kuendelea kutoa misaada huku akiendelea kuwasihi wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya wizara ya afya .
"Tuendelee kushirikiana ili kumaliza ugonjwa huu wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na kirusi cha Corona japokuwa kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa nchini tumevipokea vifaa hivi kwa mikono miwili na tutavisambaza ili kuwafikia wahusika"anasema Tutuba.
Naye Meneja Mradi wa IMPACT Mwanza Edna Selestine anasema vifaa hivyo vimenunuliwa kwa ushirikianao wa ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza hapahapa nchini huku msaada huo ukiwa ni madawa mbalimbali kwa ajili ya matibabu ya watu mwenye Corona pamoja na vifaa tiba.
"Kama wiki mbili au tatu tulitoa misaada wa vifaa kinga vya maambukizi ya Corona vyenye thamani ya Million 572,272,498 ambapo fedha hizo zimetolewa na wafadhili kwa ajili ya manunuzi ya vifaa tiba ,vitendea kazi pamoja na kuwezesha mafunzo ya watoa huduma za afya juu ya ugojwa huo pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii jinsi ya kuendelea kuelimisha jamii kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi"anaeleza Selestine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.