Ili Kupunguza vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi huduma za dharura zafanyika ili kununua vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Billion 1.5 .
Hayo yamamebainishwa na Meneja Mradi wa Impact mkoa wa Mwanza Edna Selestine alisema vifaa hivyo vimetolewa na Aga khan Development Network kwa ufadhili wa serikali ya watu wa Canada (Global Affairs Canada) kupitia mradi wa Improving Access to Reproductive Maternal and Newborn Health (IMPACT)Mwanza .
Alisema wametoa vifaa hivyo lengo likiwa ni kushirikiana na serikali katika kupunguza vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga pia mradi huo unafanyakazi katika vituo vya kutolea huduma za afya 80 ndani ya Halmashauri zote nane za mkoani humo.
" Mradi wa IMPACT umeendelea kushirikiana na Wizara ya afya ,ofisi ya Mganga mkuu Mkoa katika kuboresha huduma za dharura,afya ya uzazi,mama na mtoto ili kufikia lengo hilo mradi wa IMPACT kwa ufadhili wa Global Affair Canada umejenga majengo 27 ya kutolea huduma za mama na mtoto ikiwa ni pamoja na majengo nane yenye kufanyia upasuaji pia umewezesha upatikanaji wa vifaa tiba pamoja na thamani katika majengo hayo ili kuwezesha utoaji wa huduma zote za msingi kwa mama na mtoto" alisema Selestine.
Naye Mtendaji Mkuu Mkoa wa Mkoa wa Mwanza wa taasisi ya maendeleo ya Aga Khan Health Service ,East Africa, Sulaiman Shahabuddin alisema wamekabidhi vifaa tiba mbalimbali vikiwemo mashine nane za kutolea dawa za usingizi zenye thamani ya Million 408,618,400 kwa ajili ya kutolea huduma za upasuaji katika hospital za Wilaya za Nyamagana, Misungwi,Nansio ,Ngudu,Magu, na katika vituo vya afya Buzuruga,Kakobe na Sengerema .
Aliongeza kuwa wataendelea kushirikiana na mkoa wa Mwanza kila panapowezekana ili kuboresha huduma za afya ya uzazi ,mama na mtoto pia natoa shukurani kwa wafadhili Global Affair Canada kwa kuendelea kutuunga mkona katika jitihada hizi .
" Pia tunaimpongeza serikali kwa jitihada zote zilizofanyika katika kupunguza vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi na watoto wachangia" anaeleza Shahabuddin
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa wa Mwanza Emmanuel Tutuba alitoa shukrani kwa wadau wote waliguswa na kutoa misaada na kuunga mkono juhudi za serikali hiyo imani yao vitadunu kwa muda mrefu , aliahidi vifaa hivyo watavielekeza mahali palipokusudiwa kwani vifaa hivyo vitasaidia Jamii mzima na siyo mama na mtoto pekee .
Alisema wazo la kuwekeza Mwanza ni sahihi kwani kuna idadi kubwa ya watu kutoka mikoa nane jilani na nchi kama sita zinazoizunguka ambapo watu wake wa apata huduma mkoani humo hivyo lengo lao la kuhitaji kuboresha na kuifanya hospital hiyo kuwa ya Mkoa ni njema na lenye kuleta tija na maendeleo ya Mkoa na nchi nzima.
Naye Mganga Mkuu Mkoa wa Mwanza Thomas Rutachunzibwa alisema wameshirikiana na IMPACT takribani miaka mitano ili kutekeleza mradi wa afya ya kumsaidia mama na mtoto ikiwa ni moja ya mikakati ya Mkoa kupunguza vifo hivyo pia wamekuwa na maboresho makubwa ndani ya Mkoa na wamewashirikisha wadau wote ili kuboresha huduma ya afya ya uzazi .
Aliongeza kuwa serikali imefanya maboresho makubwa kwa takribani hospital 17 zimefikiwa pia wanaendelea kuboresha zahanati na ujenzi wa hospital za Wilaya pia kupitia mradi huo umewasaidia vituo vya kutolea huduma za afya 80 sambamba na kufanya uwekezaji wa miundombinu upande wa majengo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.