• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

ASKOFU SANGU ATETA NA RC MTANDA

Posted on: August 13th, 2024

ASKOFU SANGU ATETA NA RC MTANDA


Mhashamu Baba Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Askofu Liberatus Sangu amemtembelea Ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda mapema leo Agosti 13, 2024 kwa lengo la kumsalimia na kumkaribisha katika sherehe za uzinduzi wa Jimbo jipya la Bariadi zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Akizungumza katika kikao kifupi,  Baba Askofu amesema kama ilivyo katika upande wa serikali ambapo maeneo ya utawala huboreshwa ili kuwafikia wananchi ndivyo ilivyo pia katika upande wa kanisa hilo ambapo wanatarajia kuligawa Jimbo la Shinyanga ili kuweza kurahisisha huduma na kuwafikia waumini wao kwa karibu zaidi.

"Taratibu za maandalizi bado zinaendelea za kumkaribisha Askofu wa Jimbo jipya la Bariadi mara baada ya Baba Mtakatifu kuridhia, Mchakato pia bado na wakati wowote taarifa rasmi zitatolewa". Askofu Sangu.

Sambamba na hayo Askofu huyo pia ametumia wasaa huo kumkaribisha Mkuu wa Mkoa kushiriki katika maandalizi na ikiwezekana pia hata katika sherehe hizo wakati utakapowadia, aidha amemtaka Mhe. Mtanda kuwataarifu Wahe. Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa wa Kanda hiyo.

Kwa upande wake Mhe. Mtanda amemtoa hofu Baba Askofu kwa kumuhakikishia kuchangia kiasi cha Shilingi milioni tatu (3) katika maandalizi ya shughuli hiyo na kumuahidi kushiriki kikamilifu katika sherehe hiyo.

"Nimekuwa na mahusiano mazuri na kanisa katoliki kwa kipindi kirefu, tangu nikiwa DC kwa kipindi cha miaka saba, hata Askofu Msoganzila wa Bunda na yeye amesema ana sherehe zake hapa Mwanza nami nitamuunga mkono"  Mhe. Mtanda.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mkoa amesema yeye binafsi ana dini yake lakini serikali haina dini hivyo ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.