Balozi wa India nchini, Mhe. Sanjiv Kohli amesema taifa lao linafurahishwana namna Tanzania inavyotoa fursa na kuwalinda wawekezajinchini kitendo ambacho kimeendelea kuwa kivutio kwao.
Kauli hiyo ameitoajana mkoani Mwanza katika mkutano wa pamoja kati ya wafanyabiashara waIndia waishio Tanzania na wanachama wa Chemba yaWafanyabiashara,wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Mkoa wa Mwanza.
Kohli alisema tangumwaka 1990 hadi 2018, India imeweza kuwekeza miradi mbalimbali Tanzania ambayoinafikia Dola za Marekani bilioni 2.21 sawa na Sh trilioni 5.5 zaTanzania na kutoa ajira zipatazo 55,000 katika miradi 424.
“India ni ya taifala tano katika uwekezaji wa miradi hapa Tanzania ikitanguliwa naChina, Uingereza, Marekani na Mauritius, ukiwa India ukiulizamfanyabiashara yeyote anataka kuwekeza wapi, ataanza kuitaja Tanzania, hii niishara kwamba ni kivutio.
“Binafsinathibitisha wazi India na Tanzania tumekuwa katika ushirikiano tangu mwaka1972 ambapo hadi kufikia 2018, jumla ya wanafunzi 500 wamesomea na kupatamafunzo mbalimbali, hata katika mkutano huu wapo waliosemea kule na kuja kuwaviongozi.
“Hapa Tanzania ipobaadhi ya miradi ambayo tumeitekeleza na hata kutoa misaada katikaChuo Kikuu cha Dar es Salaam na vyuo vingine vikiwamo DIT sambamba na hospitaliya Bugando, vile vile ipo miradi ya maji kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze,mradi wa maji wa vijiji 89 vya mkoa wa Tabora katika wilayaza Nzega na Igunga,”alisema
Balozi Kohlialisema baada ya kuteuliwa kuja Tanzania amefurahi kuona wafanyabiashara waIndia wakiendelea na shughuli zao nchini bila kuwa na kikwazochochote ambapo aliahidi kuhamasisha matajiri wa taifa lao kuja kuwekeza zaidi.
Alisema baadhi yamiradi waliyowekeza nchini hawajawahi kupata hasara jambo ambalo linathihirishaushirikiano uliodumu tangu mwaka 1972, hivyo aliwahakikishia masoko kwa baadhiya bidhaa ambazo Tanzania imekuwa ikitegemea soko India.
Naye Katibu Tawalawa Mkoa wa Mwanza, Christopher Kadio ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo,John Mongella alimuomba na kumhakikishia balozi huyo kwamba Tanzaniainawakaribisha wawekezaji na kuwalinda kwa namna yoyote ili kilaupande uweze kunufaika ambapo alianisha uwekezaji unaohitahitajika kwa sasa nisekta ya kilimo na viwanda vya kuzalisha bidhaambalimbali.
Kadioalisema moja ya mikoa yenye fursa katika uwekezaji niMwanza ambayo ni kitovu cha nchi za Afrika Mashariki kutokana nauwezo wa ardhi ya kutosha, ziwa viktoria, madini, hifadhi za taifa za wanyamana mzunguko mkubwa wa fedha.
“Mwanza tunaendeleakutekeleza sera ya Tanzania ya uwekezaji ndio maana tunawakaribisha wawekezajikwa kuwa ardhi tunayo tena ya kutosha ikizingatiwa mkoa wetu ndiokitovu cha nchi za Afrika Mashariki, kupitia uwepo wa balozi wa India hapa,tunamuomba awaweleze watu wake wawekeze hasa katika viwanda, kampuni zauhandisi, hoteli na sekta ya kilimo nayo inahitaji uwekezaji.
“Ukiwekeza Mwanzaunakuwa umejiweka katikati ya soko la nchi za Afrika Mashariki, uhakika upo wakile unachokizalisha kununuliwa ukizingatia Serikali ipo kwenye utekelezaji wakuboresha miundombinu ya majini na nchi kavu sambamba na vyombo vyausafiri ikiwa lengo ni kuondoa changamoto ya mawasiliano yaliyokuwapoawali,”alisema.
Kwa upandewa Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara,wenye Viwanda na Kilimo Tanzania(TCCIA), Mkoa wa Mwanza, Dk. Elibariki Mmari alisema lengo la kukutanishwawafanyabiashara wa India na Tanzania ni kujifunza na kupata uzoefuwa kujenga miradi mikubwa.
Dk. Mmarialisema raia wa India wamepiga hatua katika masualaya teknolojia hasa upande wa uhandisi hivyo ni matarajio kwawatanzania kutumia fursa ya kushirikiana na kupata uzoefu wa ujenzi wa madarajamakubwa nchi kavu na majini, majengo marefu aina ya maghorofa.
“India na Tanzaniazimekuwa katika mahusiano ya miaka mingi hakujawahi kutokea hali ya kuteterekauhusiano wa kidiplomasia ndio maana unaona wafanyabiashara wan chihizo mbili wamekuwa na ushirikiano sana katika shughuli zao.
“Indiaimekuwa ni moja ya taifa ambalo linanunua kwa wingibidhaa kutoka Tanzania ambazo ni pamba, korosho, dengu, madini aina ya dhahabuna almasi, hivyo hivyo na sisi watanzania tumekuwa tunaagiza vitu kutoka Indiaambavyo ni nguo, dawa, gari na huduma zakibenki,”alisema.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.