Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana leo Septemba 26, 2025 amepokea wageni kutoka wizara ya madini waliopo mkoani humo kwa ziara ya mafunzo wakiongozana na ugeni kutoka nchini Malawi kwa lengo la kujifunza kupitia shughuli zinazotekelezwa na hiyo pamoja na taasisi zake.
Ziara hiyo imelenga kujifunza namna ambavyo wizara ya madini imefanikiwa katika usimamizi na urasimishaji wa wachimbaji wadogo, uendeshaji wa masoko ya madini ambapo wanakusudia kutembelea katika soko la madini na kiwanda cha kusafisha dhahabu cha kampuni ya Mwanza precious metal refinery Ltd.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.