Balozi mdogo wa Ujerumani Nchini Tanzania Mhe. Jorg Herrera kwa kushirikiana na Mwambata wa GAFTAG, Lt. Col. Thomas Nalbach amekabidhi Majengo ya Chuo cha tiba cha JWTZ Mwanza kwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Lt.Gen Yacoub H. Mohamed aliyeongozana na timu ya JWTZ .
Akipokea majengo hayo Mnadhimu Mkuu Lt. Gen Yacoub amesema amefurahishwa sana na majengo hayo na kukiri kuwa itakuwa msaada mkubwa kwa JWTZ na kuwashukuru Ubalozi wa Ujerumani kwa makabidhiano hayo.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella, aliyeshuhudia makabidhiano ya majengo hayo, amepokea Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,inayoongozwa na Mhe. Hawa Ghasia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.