Leo Agosti 30, 2025 Mwenge wa Uhuru umekagua na kuweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami (Double Surface Dressing) zenye urefu wa kilometa 0.72 unaotekelezwa na mkandarasi MS Jassle Company Ltd kwa Tshs. 474,950,400.
Akiongea na wananchi kwenye mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Bw. Ismail Ali Ussi amemtaka Mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa miundombinu hiyo kwa mujibu wa mkataba na kwa ubora unaokubalika ili barabara hizo zirahisishe mawasiliano na kusaidia kuchochea maendeleo.
Bwana Ussi ameipongeza serikali kupitia mfuko wa maendeleo ya jimbo kwa kutoa fedha nyingi chini ya usimamizi wa Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) katika kuhakikisha wananchi wa barabara za CCM-Bwawani (0.25) na Pambalu (0.47) ikiwa ni katika kuwaboreshea mawasiliano ili kuboresha huduma za kijamii.
“Serikali inatekeleza mradi huu (Barabara) na mingine mingi kwa sababu nyie wananchi mmekua tayari kupokea, hivyo nawaomba muendelee kuipenda na kuiamini serikali yenu ya awamu ya sita ambayo ipo kwa masilahi ya wananchi wakati wote na itaendelea kuwaletea miradi mingi ya kijamii.” Amesema kiongozi huyo.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mhe. Senyi Ngaga amebainisha kuwa serikali imejenga barabara hizo za mjini kati ili kuupa hadhi mji wa Sengerema na kwamba zitakapokamilika zitawasaidia wananchi kuwafikisha kwa urahisi na haraka katika maeneo ya huduma za kijamii kama hospitali na sokoni.
Awali, Meneja TARURA wa Wilaya hiyo Mhandisi Prosper Francis amefafanua kazi zilizofanyika kuwa ni Ujenzi wa kitako cha barabara (Road bed), Tabaka la chini (G15), Tabaka la kati (CM), Tbaka la juu (CRS) pamoja na tabaka la kwanza la lami (Prime-coat) na Ujenzi wa Makalavati 6 yenye kipenyo cha 900 mm.
Katika wakati mwingine Mwenge wa Uhuru umezindua Nyumba ya watumishi wa Zahanati ya Butonga (2 in 1) iliyojengwa kwa zaidi ya Milioni 102 kutoka TASAF na umeweka Jiwe la Msingi shule mpya ya Sekondari ya Isungang’holo iliyojengwa kwa Milioni 584.2 kabla ya kuweka jiwe la msingi Mradi wa Maji wa Bilioni 3.37 katika kijiji cha Sima.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.