Waziri wa viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa (Mb) amewahakikishia watanzani kuwa hakutakuwa na uhaba wa sukari tena na kuwataka wananchi wasiwe na hofu juu ya sukari na kuwaasa wauzaji kutumia bei elekezi.
Mhe.Bashungwa ameyasema hayo mara alipofika katika bandari ya Mwanza kusini na kushuhudia Shehena ya Sukari tani elfu 20 ikishushwa na meli kutoka Nchini Uganda.
Aidha ameongeza kuwa kila mwaka viwanda vyetu vya ndani vinaposimisha uzalishaji kwa ajili ya ukarabati wa mitambo huwa ilaleta changamoto lakini amemshukuru Rais, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli kwa kutambua hilo na kuona ni kipindi ambacho ndugu zetu Waislamu wapo kwenye mfungo wa Mwezi mtukufu wa ramadhani na kuhakikisha upatikanaji wa Sukari kila mahali.
"Watanzania wote nawaomba muendelee na mwezi mtukufu wa ramadhani vizuri Serikali tunahangaika ili kuhakikisha sukari inapatikana mikoa yote na kupanda kwa bei hakutakuwepo na tunaendelea kutoa wito kwa wakuu wa mikoa na Wilaya kuendelea kusimamia ukomo wa bei ambao ulitolewa na Serikali,"alisema Mhe.Bashungwa.
Naye wakala wa usambazaji Sukari kanda ya ziwa Pravin Shah amesema hakuna foleni wala uhaba wa sukari kwa sasa kwani ipo ya kutosha.
"Hakuna uhaba wa sukari hata ukitaka mifuko elfu moja na bei ni elekezi ya Serikali," alisema Shah.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amesema kama Mkoa umejipanga ili kuhakikisha sukari hiyo inawafikia wananchi kwa bei elekezi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.