Benki ya Damu salama Kanda ya Ziwa imeshauriwa kuja na mkakati wa kuwashirikisha Viongozi kuanzia ngazi ya Mkoa kushuka chini katika kuhamasisha uchangiaji wa rasilimali hiyo na kufikia malengo ya Mkoa.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani iliyofanyika leo Mkoani Mwanza, Ngusa amesema zoezi hilo la kuwashirikisha Viongozi na kada mbalimbali litakuja na matokeo chanya kutokana na watu kuhamasika.
"Mkoa wetu kabla ya Sensa ya mwaka huu tuna idadi ya watu Milioni tatu na nimesikia bado tuna changamoto ya kufikia malengo ya damu Mkoa, tushirikiane vizuri na kufika mahitaji ya chupa 32,400 kwa mwaka zinazohitajika Mkoani."
Ndugu Samike amesema suala lililopo mbele yetu ni kasi na mipango imara ya uhamasishaji ikiwemo kutumia fursa ya mikusanyiko ya watu katika hafla mbalimbali pia na sehemu za watu kufanyia ibada.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dktr. Thomas Rutachunzibwa ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiboresha Benki hiyo ya Damu Kanda ya Ziwa kwa kuleta mashine za kisasa za Damu na mazao yake.
Katika Maadhimisho hayo Katibu Tawala amewakabidhi zawadi ya Majiko ya Gesi wadau waliochangia damu kwa muda mrefu Mkoani Mwanza
Maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Ulimwenguni hufanyika kila tarehe 14 Juni ikiwa ni heshma ya kutambua mchango wao kwa jamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.