*Bilioni 25 kunufaisha wavuvi, Wafugaji wa samaki 2000 kanda ya ziwa:Waziri Ulega*
Wanufaika 2000 kutoka sekta ya Uvuvi kutoka mikoa ya Mwanza,Kagera,Mara,Geita na Simiyu watanufaika na mradi wa kisasa wa ufugaji wa samaki na Uvuvi kwa kukabidhiwa boti za kisasa na vizimba ukiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita ya kuinua uchumi wa wananchi.
Akizungumza leo Mkoani Mwanza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati wa ziara yake ya kukagua Boti 55 na Vizimba 273 zitakazotolewa kwa makundi mbalimbali,amesema mkakati huo ni uwezeshaji kwa wananchi kwa vitendo kwa mkopo nafuu usiyo na riba.
"Hii haijawahi kutokea ni kwa mara ya kwanza Serikali ya Rais Samia inafanya jambo hili kubwa, unakabidhiwa boti ya kisasa yenye vifaa vyote muhimu vikiwemo vya kubaini sehemu walipo samaki na mahali pa kuwahifadhia",Mhe.Ulega.
Amebainisha baadhi ya wafugaji wa samaki wa vizimba watakabidhiwa pia boti kwa ajili ya kuwasaidia safari ya kwenda eneo la mradi wao na wavuvi watakabidhiwa boti za ukubwa tofauti kulingana na ombi lao.
"Nimefarijika kuziona boti hizi na vifaa vyake,hivi karibuni Mhe.Rais amekabidhi boti za uvuvi huko mkoani Pwani kwani Serikali imetoa jumla ya boti 165 na vizimba 165 kwa wanufaika upande wa Bahari na Maziwa,"amesisitiza Waziri Ulega.
Aidha amesema fedha hizo zimetolewa na Serikali na kukabidhiwa Benki ya Kilimo ya TADB na baada ya miaka minne itaanza kupokea marejesho ya mkopo huo na umetolewa muda huo ili kuwapa nafasi wanufaika kujipanga vizuri na miradi yao.
Amewataka pia wanafukaika wote watembelee na kujionea vyombo vyao vilivyopo maeneo ya Chuo cha Uvuvi Nyegezi kabla ya Mhe.Rais hajawakabidhi rasmi.
"Wanufaika wa mradi huu ni vikundi vya ushirika 23,Kampuni 10, na watu 28 huku Mwanza wakiwa na wanufaika 29 ambao ni wengi zaidi kulinganisha na mikoa mingine,"Nazael Mandala,Mkurugenzi Ukuzaji Viumbe maji,Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Mradi huu utawasaidia wanafaika hao kuvuna samaki zaidi ya Tani elfu tano hadi kumi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.