Shirika lisilo la kiserikali la Blue Victoria limezindua miradi miwili bunifu inayolenga kulinda mazingira ya Ziwa Victoria, ikiwemo mradi wa ufuatiliaji wa vifereji kwa kutumia teknolojia ya kisasa na mradi wa kuondoa nyavu zilizotelekezwa majini, maarufu kama Ghost Nets.

Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa ufuatiliaji wa mifereji kwa kutumia teknolojia ya kisasa ambao utasaidia kubaini vyanzo vya uchafuzi vinavyoingia ziwani, na mradi wa kuondoa nyavu zilizotelekezwa (Ghost Nets) ambazo zimekuwa tishio kwa samaki, wavuvi na bioanuai ya ziwa hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Katibu Tawala anaeshughulikia Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Mwanza Bw. Peter Kasele amelipongeza shirika la Blue Victoria kwa ubunifu na mchango wake katika juhudi za kulinda mazingira, akisema miradi hiyo ni mfano wa ushirikiano mzuri kati ya sekta binafsi na serikali katika kutatua changamoto za kimazingira.

Bw. Kasele amesema miradi hiyo imekuja ndani ya muda muafaka kwakua kiferezi ni tukio la kiasili ambalo limekua changamoto ambayo inasababisha samaki kufa kwa wingi hali ambayo inahatarisha shughuli za uvuvi.

"Matukio ya kiferezi huleta taharuki na hasara kwa wavuvi na wafugaji wa samaki na madhara kwa mazingira ya ziwa kwakua samaki wanakufa". Amesema Bw. Kasele.
Aidha, ameongeza kuwa jitihada hizo za sekta binafsi kuiunga mkono serikali inachangia kuimarisha uvuvi endelevu, uhifadhi wa biyoanuia na matumizi bora ya teknolojia katika kusimamia mazingira ya asili.

Naye, Mfawidhi wa Uvuvi Kanda ya Ziwa Victoria amesema anawashukuru wadau wa maendeleo kwa pamoja kwa kuziunga mkono jitihada za Serikali na kushirikiana nayo katika kuikuza sekta ya uvuvi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Blue Victoria Festus Massaho amesema teknolojia wanayoizindua inaenda kutatua changamoto zitakazojitokeza katika shughuli za uvuvi na maisha ya viumbe maji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.