BODABODA MWANZA WALAANI MAANDAMANO YA CHADEMA YA FEBRUARI 15
*Wasema wanajivunia kazi yao kwenye utulivu na amani*
*Wasema wanaomboleza msiba wa aliyekuwa Waziri Mkuu*
*Walaani kiongozi wa CHADEMA kuita bodaboda ni kazi ya laana*
Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Jijini Mwanza wamelaani maandamano yanayoratibiwa na Chama cha Demekrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Mwanza mnamo tarehe 15/02/2024 huku wakibainisha kuwa hayana afya kwa Taifa.
Wamesema, hawako tayari kuandamana badala yake wataendelea kushiriki kikamilifu maombolezo ya siku 5 yaliyotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kifo cha aliyekua Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa na si mambo mengine ambayo hayana uungwana.
Makamu Mwenyekiti wa Bodaboda Mwanza John Razaro amesisitiza kwa kusema kuwa hawawezi kuandamana kutokana na msiba wa kiongozi ambaye alikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa.
Vilevile, wamesema kwa sauti moja wanalaani vikali maandamano hayo na kuahidi kutojihusisha nayo kabisa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo pia kauli iliyotolewa na kiongozi wa upinzani siku za nyuma ikieleza kuwa kazi ya bodaboda ni kazi ya laana.
"Kuna kiongozi aliwahi kusema kuwa bodaboda ni kazi ya laana hivyo haifai kufanywa na binadamu, kauli hii ilituumiza sana na hatuwezi kuungana na watu ambao wameona kazi yetu ni ya laana ikiwa kazi hii inasaidia maisha ya familia zetu’’ , Lazaro.
Naye, Mororo Daniel ambaye ni mmoja wa wanachama wa umoja wa bodaboda Buhongwa ameeleza kuwa haoni tija ya kujiingiza katika maandamano hayo kwani Serikali imekuwa ikifanya mambo mengi mazuri ambayo wananchi wamekuwa wakinufaika nayo ikiwemo ujenzi wa hospitali, shule pamoja na miundombinu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.