Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Tanzania CCM amefanya ziara ya kikazi mkoani Mwanza ikiwa ni ziara yake ya Kwanza tangu ateuliwe kuchukua nafasi hiyo kitaifa
Akiwa Katunguru wilayani Sengerema Dkt Bashiru amekagua eneo ambalo wanatarajia kujenga chuo cha uongozi. Hata hivyo pia Katibu Mkuu amewahasa wana CCM wote Nchini kuwa na Umoja na kumaliza makundi na migogoro ya kimaslai ambayo hupelekea CCM kuvurugika na kuwafanya wananchi kukichukia Chama.
Dkt Bashiru amesema CCM kwa sasa hivi kimekuwa ni chama ambacho heshima yake ya awali inarudi kutokana na Viongozi wakuu wa Chama kusimamia misingi iliyowekwa na waasisi wa Chama Mwl Nyerere na Sheik Abeid Aman Karume.
"Kama chama tumejipanga kuadhimisha miaka Ishirini ya Kifo cha Mwl Nyerere kwa kutangaza ndani na Nje ya Nchimafanikio makubwa yaliyofikiwa na serikali ya awamu ya Tano .Mengi Miradi mikubwa na mambo makubwa yanayotekelezwa yalikuwa ni maono ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere " alisema Dkt Bashiru
Miradi mikubwa inayotekelezwa ni Pamoja na Ujenzi mkubwa wa Mradi wa Umeme Mto rufiji "Stiglers Gauge" ujenzi wa reli ya kisasa , ufufuaji wa shirika la Ndege, utoaji wa elimu Bure,Ulinzi wa rasilimali zetu, Maadili ya Viongozi na watumishi wa Umma.
Hata hivyo Katibu Mkuu amepata fursa ya kutembelea upanuzi wa Barabara Mjini mpaka Uwanja wa Ndege, Upanuzi wa kiwanja cha ndege
.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.