Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ndugu Balandya Elikana, leo Januari 28, 2026, ameupokea ugeni kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ) uliowasili mkoani humo kwa shughuli maalumu.

Ugeni huo wa Wizara ya Ulinzi na JKT umefika Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kukagua na kufanya tathmini ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya kimaendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Ukaguzi huo unalenga kuona hatua iliyofikiwa ya miradi hiyo na kwa namna gani miradi ya kimkakatiā inaweza kutumika na Wizara ya Ulinzi, JKT na JWTZ kwa ujumla katika kipindi Cha majanga ya asili na yasiyo ya asili na operesheni mbalimbali za kijeshi.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.