CHANGAMKIENI FURSA ZA UWEKEZAJI MWANZA:RAS BALANDYA
Kampuni za simu nchini zimeshauriwa kuwekeza katika mkoa wa Mwanza kwa lengo la kuuza bidhaa zao ili kuweza kuinua mawasiliano kwa wakazi wa mkoa huo.
Rai hiyo imetolewa leo Juni 14,2024 na Katibu Tawala Msaidizi,Mipango na Uratibu Bw.Henry Mwaijega kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza wakati wa ufunguzi wa duka la kampuni ya simu ya Tecno katika eneo la Nyerere road.
Mwaijega amesema kwa upande wa uwekezaji wa maduka ya kampuni za simu katika mkoa wa Mwanza bado maduka mengi yapo katika maeneo ya Mwanza mjini haswa Wilaya za Ilemela na Nyamagana.
Ameshauri ni vyema makampuni ya simu yafunge maduka ya bidhaa zao katika maeneo ya wilaya za Sengerema na Ukerewe ili kufikisha huduma za mawasiliano kwa wakazi wengi zaidi katika mkoa wa Mwanza.
‘’ Kampuni za simu zinapofungua maduka ya bidhaa zao katika maeneo tofauti hapa katika mkoa wa Mwanza, inasaidia kuweza kutengeneza ajira katika sehemu husika pamoja na kukuza mawasiliano na kuinua uchumi’’ amesema Mwaijega
Amesema Rais Samia Suluhu amewezesha mazingira mazuri ya uwekezaji, hivyo wawekezaji wasiogope kujitokeza na kuwekeza.
Katika hatua nyingine, Mwaijega ameipongeza kampuni ya simu ya Tecno kwa kuweza kuleta bidhaa bora na za bei nafuu na kila mmoja anaweza kununua.
Amesema Sekta ya Mawasiliano nchini ni moja ya sekta muhimu sana katika kuweza kuinua uchumi.
Naye meneja wa kampuni ya simu ya Tecno Kanda ya Ziwa, Edward Mathias amesema kuwa kampuni yao imefanikiwa katika mwaka huu kufungua maduka mbali mbali ya bidhaa zao katika maeneo ya Zanzibar,Mwanza Dodoma na Mbeya.
Amesema kampuni yao inauza simu mbalimbali pamoja na laptop
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.