Vyumba vitano vya madarasa vyajengwa ili kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi darasani hali hiyo itakayoboresha mazingira ya kujifunza na walimu kufundisha vyema ili kupandisha ufaulu wa wanafunzi na kuhamasisha mahudhurio darasani.
Akisoma taarifa fupi ya mradi huo Mkuu wa shule ya msingi Iseni “B” Donald Jovine alisema shule hiyo ina wanafunzi 1390 ambapo awali ilikuwa ikikabiliwa na changamotoya madarasa hivyo mradi huo umegharimu Million 79.16 kutoka katika vyanzo mbalimbali ambapo Mhe.Rais alichangia million tano, mbunge wa jimbo hilo million mbili ,Naibu Waziri wa maji million moja na halimashauri hiyo ikitoa millon 71.16.
“Awali tulikabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo tunaishukuru Serikali kwa sababu watoto wetu hawataweza kubanana tena kama ilivyokuwa awali “.alisema Jovine.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku mbili ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekeleza katika wilaya ya Nyamagana Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella aliwataka walimu kuongeza jitihada katika ufundishaji ili kuleta matokeo yaliyo bora na yenye tija ,huku akiwataka wanafunzi hao kuwa wasikivu kwa walimu na wazazi wao , kuwa na hekima na kuepukana na watu wenye nia ya kuwapotosha na kuwapotezea dira ya kufikia malengo yao .
“Ukiona mtu akakuamba mambo ya hovyo kamwambie mwalimu au mzazi kuna majitu mtaani yana akili mbovumbovu yanataka kuwaharibu akili za watoto usikubali, akija mkaka au mdada anakuambia maneno au mambo ya hovyo kataa kimbia alafu nenda kamwambie mkubwa aliyeko karibu yako na sisi mkitoa taarifa, hayo majitu tutayakamata na kuyashugulikia”alisema Mhe.Mongella.
Ester Joel ni mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo alisema wanamshukuru Mungu kwa zawadi ya mema yote yanayotokea shuleni hapo pamoja na Serikali kwa kuona changamoto yao hivyo wanaahidi kujituma katika masomo na kuyatunza vyema majengo hayo kwa faida yao na kizazi kijacho.
Mradi huo waujenzi wa vyumba vya madarasa uliasisiwa na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli Desemba 7 mwaka jana ambapo utekelezaji wake ulianza Desemba 8 mwaka jana huku ukitarajiwa kukamilika February 18 mwaka 2020 ambapo kwa sasa mradi huo upo katika hatua yaukamilishaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.