Mwezi Novemba na Desemba 2019 pengine ni kati ya vipindi ambavyo mkoa wa Mwanza umeshuhudia na kupokea ugeni mkubwa Kitaifa na Kimataifa.
Ni kipindi hicho ndipo maadhimishi ya wiki ya siku ya Ukimwi yalipofanyika jijini Mwanza ikiwaleta pamoja viongozi wa Kitaifa na Kimataifa.
Kitaifa walikuwepo Mawaziri, Watendaji wakuu wa taasisi zinazohusika na mapambano dhidi ya Ukimwi, wasanii pamoja na wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya Ukimwi (UNAIDS), wanawake (UN WOMEN na kazi (ILO).
Kilele cha maadhimisho hayo vilivyofanyika katika viwanja vya Rock city Mall vilishirikisha watu kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo vijana na wazee wake kwa waume.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ni kati ya viongozi wa Kitaifa waliofika Mwanza katika wiki ya siku ya Ukimwi kwa ajili ya kuhudhuria kongamano maalum lililoandaliwa na Kamati ya kupambana na Kifua Kikuu (TB).
Kongamano hilo lilijumuisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini na wastaafu wakiongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda.
Orodha ya viongozi wa Kitaifa waliofika Mwanza kuanzia maadhimisho ya Ukimwi pia wamo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu) Jenista Mhagama na Katibu wa Baraza la Ulama Taifa Sheikh Hassan Said Chizenga.
Pia walikuwemo Makamu wa Pili wa Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa Tanzania (CCT) Jacob Chimeledy na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wabunge walio kwenye mapambano TB nje ya Bunge, Osca Mkasa.
Latola ngazi ya Kimataifa,
Mwanza pia imewapokea wawakilishi wakazi wa mashirika na taasisi za Umoja wa Mataifa walioongozwa na Mwakilishi mkazi wa UN AIDS, Dk Leo Zekeng.
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi yameambatana na maadhimisho mengine ya siku 16 ya kupiga vita vitendo vya ukatili na unyanyasaji kujinsia dhidi ya wanawake na watoto ambapo hoja ya kuwepo pete tegesha za uchumba miongoni mwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu iliibuliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Kivulini, Yassin Ally.
Taarifa za pete tegesha za uchumba na ndoa za kuwalaghai wanafunzi wa kike zimeigutusha Serikali ambayo kupitia Waziri Mhagama imetangaza kuitisha kikao cha wadau wote ifikapo Januari, 2020 kujadili na kutafutia ufumbuzi suala hilo.
Akihutubia kilele cha siku ya Ukimwi katika viwanja vya Rock city Mall kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri Mhagama akautaarifu umma kuwa kikao hicho kitaandaliwa kupitia uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Wazira ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.