Daraja la mto Simuyu lililoko Wilayani Magu, barabara kuu ya Mwanza-Musoma limeharibika kutokana na uchakavu jambo lilipelekea vyuma kukatika lita fungwa kwa muda wa siku 10 ili kupisha utekelezwaji wa matengenezo makubwa .
Akiwasilisha taarifa ya ufungwaji wa daraja hilo Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa M. Rubirya alisema watafunga barabara ya Mwanza- Musoma kuanzia Machi 8 hadi 18 mwaka huu ili kupisha matengenezo makubwa ya daraja hilo.
Mhandisi Rubirya ameongeza kuwa wameamua kufanya matengenezo ya haraka ili kujiepusha na hatari zitakazoweza kujitokeza kwa sababu kuchelewa kwa ujenzi huo yaweza kuwa hatarishi kwa watumiaji wa barabara hiyo .
Aliongeza kuwa barabara hiyo itafungwa ili kupisha matengenezo kuanzia saa tatu usiku hadi saa 11 asubuhi pia aliomba ushirikiano wa Jeshi la polisi katika kutekeleza kazi hiyo.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa daraja hilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella alisema kutokana na changamoto hiyo njia zitafugwa kwa muda uliopangwa kwa siku kumi ili kupisha matengenezo hayo.
Alisema Serikali inampango wa kujenga daraja jipya hivyo hatua zinazofanyika sasa ni za muda mfupi, aliwataka wananchi kuwa wavumilivu waweze kuboreshewa njia itakayowanufaisha na kuendeleza ujenzi wa taifa.
" Hali halisi ilivyo na nyie mmeiona ninachowaomba muwe wavumilivu ujenzi ufanyike ili kuepusha madhara makubwa ya baadaye" alisema Mhe.Mongella.
Lusia Isack ni mmoja wa wakazi wa Magu akizungumzia adha hiyo alisema wanakuwa wa hofu kila wanapopita kwenye daraja hilo hasa wanapofika katikati hivyo wanaishukuru Serikali kwa kuliona hilo kwani wameweza kutatua changamoto hiyo kabla haijaleta maafa.
"Hili daraja ni bovu sana ata ukiwa umebebwa kwenye baiskel ukifika katikati daraja linaanza kucheza sasa ukiwa kwenye gari unawaza sijui nitapita salama kwa sababu likidondoka tu sizani kama kuna mtu atakayepona kinachobaki ni kuomba Mungu wakitutengenezea watakuwa wametusaidia sana." alisema Isack.
Hata hivyo daraja hili lililojengwa mwaka 1962 limeanza kuonyesha nyufa baada ya vyuma vilivyokuwa vinalishikilia kukatika jambo hilo limejenga hofu kwa Serikali na watumiaji wa njia hiyo harakati za haraka zinafanyika ili kubadilisha vyuma hivyo .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.