Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amefungua warsha ya Utoaji Elimu kuhusiana na huduma za hali ya hewa zinazozingatia athari iliyofanyika Mkoani Mwanza katika Ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu.
Akifungua Warsha hiyo Mhe.Mongella amesema takribani nusu ya wakazi wa maeneo ya jirani wanategemea zaidi shughuli za ubuvi na kilimo hivyo taarifa ya hali ya hewa ni muhimu sana katika kuimarisha maisha ya yananchi na mali zao kwa wengi hutegemea ziwa victoria.
"Tutajitahidi idara ya Uvuvi na Mkuu wa idara ya Kilimo wapate simu ifikapo tarehe 1.12 ili kupata taarifa za hali ya hewa kila siku na kuziwasilisha kwenye mamlaka mbalimbali hii itapelekea kupunguza maafa,"alisema Mongella.
"Swala la kutambua hali ya hewa ni muhimu zaidi TMA muone umuhimu wa kuhusisha viongozi ngazi ya chini ili wafikishe kwa wananchi,wale watu wakipewa uelewa wa kawaida utawasaidia kujiepusha na majanga,
"Tunachangamoto nyingi katika ziwa letu hivyo kwa kuwalenga wavuvi itasaidia kupunguza madhara yanayojitokeza kutokana na kutopata taarifa za hali ya hewa,"alisema Mongella.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA)Dkt. Agness Kijazi amesema ni vizuri kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaoyolewa kwa masaa kwa sababu hali ya hewa hubadirika mara kwa mara hasa kwa wale walio karibu ya ziwa na bahari.
"Hali ya hewa hasa maeneo ya maziwa hubadirika mara kwa mara hivyo niombe mfatilie sana ili hali inapobadirika mnakuwa na taarifa sahihi,hii itawasaidia kuendelea na shughulia au kuacha hadi hali itakapobadilika, aliaema Dkt.Agness.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema Boniphace M.Mafuru amesema TMA imewasaidia sana kwani majanga mbalimbali yamepungua kwa kupata taarifa za mamalaka na kupashana Habari.
"Changamoto tunayoipata tuna simu 1 na tuna jumla ya vikundi 33 hivyo inakuwa ngumu kwa kutumia simu 1 tu kwa makundi yote", alisema Mafuru.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.