Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa huo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa Maono ya kuitangaza nchi kwa kuamua kufanya filamu ya ROYAL TOUR ambayo imeitangaza nchi kwa viwango vya kimataifa.
Amebainisha hayo kwa furaha kwenye viwanja vya Rock City Mall leo alasiri Juni 18, ,2022viwanjani Rock City Mall wakati wa Utambulisho rasmi wa Filamu ya ROYAL TOUR kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza hafla iliyotanguliwa na Maandamano adhimu ya maelefu ya Wananchi.
"Tanzania imefunguliwa na Mwanza imefunguka hadi lengo la kupokea wageni kwenye kisiwa cha Saanane imeshavunja rekodi, wageni hao wote wamewapata wana mwanza kwa kufanya nao biashara mbalimbali zikiwemo za mamalishe na wachuuzi." Mkuu wa Mkoa.
Ameongeza kuwa uwepo wa filamu ya ROYAL TOUR wananchi wa Mwanza wamefarijika sana na sasa hivi wananchi wa Mwanza ni wakati wa kutalii na kupumzika kwenye hifadhi na vivutio vilivyopo Mkoani hapo kwani baada ya kazi mtu anakwenda kisiwa cha Saanane anabarizi anawaona na Simba.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Julius Peter amebainisha kuwa pamoja na kuitambulisha Nchi kupitia Filamu ya Royal Tour Mhe Rais anawapenda watanzania na wana Mwanza na amewaletea zaidi ya Shilingi Bilioni 600 kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Bilioni 383 kwenye miradi ya kimkakati.
"Afisa Utalii Mwandamizi Mkuu wa Kanda, Bi Dainess Kunzugala amesema kuwa Sekta ya Utalii inachangia uchumi wa Nchi yetu kwa asilimia 17 na kwa asilimia 25 kwa fedha za kigeni na Mwanza ni kitovu cha utalii kwa kanda ya ziwa kwani ndipo sehemu ya katikati kufika hifadhi mbalimbali kama Serengeti na Burigi Chato.
"Sekta ya Utalii ni sekta muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, tunamshukuru sana Mhe Rais kwa kuitangaza nchi kupitia filamu ya Royal Tour ambayo ameifanya yeye mwenyewe na kwa sasa tunapokea watalii wapatao milioni 1.5 na kupitia filamu hii tunatarajia wataongezeka hadi milioni 5." Amebainisha.
Kabla ya Uzinduzi rasmi wa filamu hiyo, wananchi wa Mkoa wa Mwanza walipata fursa ya kuangalia burudani kutoka kwa wasanii wa nyimbo na maigizo na ngoma za asili.
_Mwisho_
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.