Wananchi wa Kisiwa cha Maisome na Kaunda watakiwa kuwa wavumilivu kwa changamoto walionayo baada ya gati la kivuko cha mv tegemeo kilichokuwa kikiwaunganisha kukatika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivyo serikali inashughulikia harakati za kuwatengenezea kivuo hicho.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella wakati wa ziara yake ya kukagua uharibifu wa miundimbinu mbalimbali ya barabara na madaraja yaliyokatika kutokana na mvua katika wilaya ya Sengerema na Buchosa.
Kwa upande wao Wakala wa Ufundi na Umeme ( TEMESA )wameleta mainjinia kuona kitu gani kinaweza kufanyika kwa haraka ili ushukaji na upandaji kwenye kivuko uwe rahisi na salama.
Pia aliwataka mawakala hao kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuondoa changamoto hiyo na kuongeza kuwa itakuwa ni Serikali ya ajabu baada ya kuona changamoto hiyo alafu wakataka kurahisisha mambo,uwekwaji wa ratiba ya kivuko hicho uzingatiwe ili kuwasaidia wananchi.
“Mimi nimekuja nimeona kweli ni changamoto kuna wazee wanasema jambo hilo halijawahi kutokea hivyo tushukuru Mungu kwa baraka ya mvua lakini tuitumie vyema kwa kulima ili kupata mazao mengi na ya kutosha inawezekana anatujaribu ili kuona watu wana bidii gani haya mengine Serikali inayashughulikia ”alisema Mhe. Mongella.
Pia aliwataka TEMESA kujenga banda la watu kusubilia usafiri na choo hivyo kufikia juni 1 mwaka huu viwe vimejengwa, sambamba na kuweka ratiba ya kivuko inayoeleweka pamoja na gharama za mizigo na nauliu na kuachana na tabia ya kutamka bei pasipo kuwa na mpangilio.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Dkt. Emmanuel Kipole alisema, kivuko hicho kimekuwa kikitoa huduma katika mikoa miwili kati ya Geita na Mwanza, ila kutokana na changamoto hiyo ratiba imebadilika ya shughuli za usafirishaji wa eneo hilo ambapo kivuko kinatakiwa kusimama kabla ya saa 12 :30 jioni ili wanaichi waweze kupita wakati wa mwanga ili kuondokana na changamoto wa uwepo wa wanyama pori kama kiboko na mamba katika eneo.
“Wananchi wanaendelea kutupa ushirikiano pia kwa hii changamoto ya kuwepo kwa wanyama wanaowadhuru taarifa zimefika kwenye kikosi cha wanyama pori watakuja kufanya jukumu lao na kukabiliana na wanyama hao na kuleta amani kwa wananchi”alisema Dkt. Kipole.
Samsoni Nyanda na Marco Lufungulo ni Baadhi ya wakazi wa maeneo hao walisema kitendo cha gati ilo kuzingirwa na maji baada ya kina kuongezeka kimewajengea hofu kubwa ya kupoteza maisha wakati wanapo kwenda kupata huduma hiyo, pia ikidhaniwa eneo hilo kuwepo wanyama wakali aina ya viboko na mamba.
Aidha, waliiomba Serikali kuharakisha marekebisho ya gati la kivuko hicho kinachofanya safari zake kati kaunda, maisome na mkoa wa geita kisiwa cha nkome, baada ya kujaa maji kutokana na kina kuongezeka kitendo kinachopelekea kuhatarisha maisha yao.
Kivuko hicho cha mv tegemeo kilizinduliwa na mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania September 26 mwaka 2014.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.